Mnamo tarehe 04.11.2016 majira ya saa 23:30 usiku huko katika Shule ya Sekondari Isuto iliyopo Kijiji na Kata ya Isuto, Tarafa ya Isangati, Wilaya ya Kipolisi Mbalizi, Mkoa wa Mbeya, askari wawili wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya waliofahamika kwa majina ya 1. H.4925 PC PETRO OSCAR MAGANA wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Mbeya na 2. J.1422 PC LUKAS JOSEPH NG’WEINA wa Wilaya ya Kipolisi Mbalizi walituhumiwa kuwafanyia vitendo vibaya kinyume na maadili wanafunzi wa kike wa kidato cha nne wa Shule hiyo. 
Inadaiwa kuwa, askari hao kwa pamoja wakiwa kwenye ulinzi wa mitihani ya kitaifa ya kidato cha nne 2016 waliwatoa kwenye Hostel wanafunzi wa kike kwa kile walichodai kupiga kelele. 
Baada ya kuwatoa wanafunzi hao, waliwapeleka eneo la kufoleni na kuanza kuwapa adhabu mbalimbali ambazo ni kupiga push up, kuruka kichura, kushika masikio na kuwachapa viboko sehemu za makalio vitendo vilivyowasababishia maumivu makali na kupelekea baadhi ya wanafunzi hao wa kike kuondoa na kuelekea nyumbani kwao. 

Kufuatia vitendo hivyo, Mkuu wa Shule hiyo aitwaye ROSE MZEE DIHEMBE alitoa taarifa kwa uongozi wa Wilaya ambapo taarifa zilifika kwa uongozi wa Mkoa ambao mara moja walifika eneo la tukio na kuchukua hatua za awali ikiwemo kusikiliza malalamikio hayo ya tukio na kuwaondoa askari waliolalamikiwa na mwisho kuchukua hatua za kinidhamu zilizopelekea kufukuzwa kazi askari hao. 
Hata hivyo, kutokana na vitendo walivyovifanya askari hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.  
WITO: 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishna wa Polisi DHAHIRI A. KIDAVASHARI anatoa wito wananchi waendelee kuliamini Jeshi la Polisi kwamba halitafumbia macho vitendo vya askari vinavyokwenda kinyume na maadili ya kazi yao. Pia vitendo vinavyokwenda kinyume na sheria za nchi. Aidha Kamanda KIDAVASHARI anaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa ya vitendo vyote vya uhalifu vinavyotendwa bila kujali vinatendwa na askari au wananchi wa kawaida ili hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa. 

Imesainiwa na:
[DHAHIRI A. KIDAVASHARI - DCP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...