Familia ya Kiluvia inasikitika kutangaza kifo cha baba yao mpenzi Mzee Hamadi Kiluvia (pichani) kilichotokea jana  alfajiri jijini Dar es salaam. Habari ziwafikie ndugu, jamaa, majirani na marafiki popote pale walipo.
Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Regent Estate mtaa wa Migombani nyumba namba 72 ambapo ndipo ulipo msiba.

 Msibani hapo ni hatua chache kutoka kituo cha mafuta cha Oil Com Victoria house, ila ili kufika unafuata barabara ya Mikocheni kwa Kairuki hadi njia panda ambapo unakata kulia na mbele tena unakutana na barabara inayotoka kwa JK  ambapo unakata tena kulia. Hatua chache mbele  utakuwa umefika.

Marehemu Mzee kiluvia atakumbukwa kama mmoja wa viongozi wa zamani serikalini na michezoni, ambapo katika uhai wake aliwahi kuwa mkuu wa Wilaya, mmoja wa viongozi wa chama cha mpira wa miguu cha FAT enzi hizo pamoja na kuwa kiongozi aliyeheshimika sana katika klabu ya Yanga.

UPDATES:  Mwili wa marehemu utapelekwa msikiti wa Regent Estate Ijumaa  sita kamili mchana kwa ajili ya kuswaliwa baada ya swalat'Jumaa. Kisha utapelekwa nyumbani kwake kwa ajili ya taratibu za mwisho kabla ya  kuanza safari ya kupelekwa Usangi, Same, mkoani Kilimanjaro kwa mazishi ambayo yanayotarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi saa saba mchana.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu baba yetu mahala pema peponi - Amin.

Matokeo ya Utafutaji



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...