Asasi Ya Vijana, Tanzania Youth Vision Association kwa Kushirikiana Na International Republican Institute zimetoa mafunzo ya kuboresha Uwezo wa Vijana kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba nchini katika visiwa vya Unguja na Pemba, Zanzibar.

Mafunzo hayo yameweza kufikia vijana 250 kwa njia ya Warsha na Vijana na wananchi zaidi ya 200,000 kupitia mitandao ya kijamii.

Ndugu Nasser Mtengera (Mkuu wa Idara ya Habari na Utafiti, TYVA) alielezea Lengo kuu la Mafunzo hayo ni kuongeza uelewa na ushiriki wa Vijana katika mchakato wa Mabadiliko ya Katiba. Katika ufunguzi wa mafunzo hayo Chake chake, Pemba Mheshimiwa Zainab Mussa Bakari (Mbunge) alibainisha kuwa wananchi wana haki ya kikatiba ya kushirikishwa katika mchakato wa katiba mpya na kusema nini wanachotaka kiwemo ndani ya katiba.

Mwanaharakati Na Mtetezi wa HAKI za Binadamu ndugu Deus Kibamba (Mwenyekiti - Jukwaa la Katiba Tanzania) alipata kuwaelezea washiriki wa mafunzo hayo historia ya mchakato wa mabadiliko ya Katiba, Ushiriki wa wananchi katika mchakato wa Katiba, hatua muhimu katika Mchakato wa utengenezaji Katiba, Mambo ya Msingi yaliyomo katika Katiba inayopendekezwa na Mambo muhimu kuelekea kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la katiba Zanzibar, Profesa Abdul Shariff akizungumza kuhusu umuhimu wa asasi za kiraia kutoa elimu juu ya Katiba Pendekezwa katika kongamano lililofanyika Unguja lililoandaliwa na Taasisi ya Vijana ya TYVA pamoja  na IRI.
 Mbunge wa Viti maalum Pemba-Zanzibar, Mheshimiwa Zainabu Mussa Bakari akizungumzia Haki na Wajibu wa mwananchi Kikatiba wakati wa ufunguzi wa Kongamano lililowashirikisha vijana mbalimbali kutoka kisiwani Pemba ili kujadili katiba mpya lililoandaliwa na Taasisi ya Vijana ya TYVA pamoja  na IRI.
Baadhi ya vijana wakipitia katiba wakati wa kongamano lililowakutanisha vijana hao ili kujadili haki na wajibu wa wananachi katika katiba mpya.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...