Na: Frank Shija & Daud Manongi, MAELEZO.

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limeanza kutekeleza agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufu la kufikisha umeme kwenye kiwanda cha kusindika matunda cha Bakhressa Food Product kilichopo Mwandege mkoani Pwani.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Kaimu Meneja Uhusiano wa Tanesco Makao Makuu, Leila Muhaji amesema kuwa agizo hilo limeshaanza kutekelezwa katika hatua mbalimbali na kuahidi kuwa litakamilika kwa wakati.

Muhaji amaesema kuwa agizo linapotolewa na Mhe. Rais kinachobaki ni utekelezaji tu, hivyokufuatia agizo hilo Tanesco wameanza kufanya utekelezaji kwa kuchukua hatua kadhaa ili kuhakikisha wanakamilisha kulinga na wakati kama agizo linavyosema.

“Utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais unaendelea na hadi kufikia mwezi Desemba tutakuwa tumefikisha umeme katika kiwanda hicho”. Alisema Bi. Muhaja.Aidha alitumia fursa kutoa rai kwa uongozi wa kiwanda hicho kuanza uzalishaji punde umeme utakapofika kiwandani hapo ili kuongeza uzalishaji.

Kwa upande wake Meneja Ushirikiano wa Jamii wa Kiwanda cha Bakhressa Food Product Hussein Sufian Ally amesema kuwa wanamshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kuona umuhimu wa kupelekewa umeme kiwandani hapo.

Aliongeza kuwa utekelezwaji wa agizo hilo utakapo kamilika utasaidia kuongeza uzalishaji na kupunguza gharama ambazo kwa sasa zinachangiwa na matumizi ya Jenereta katika kuendeshea uzalishaji wa Kiwanda hicho.

Utekelezaji huu umefutia agizo la Rais alilolitoa tarehe 06/10/2016 wakati wa uzinduzi wa Kiwanda cha kusindika matunda cha Bakhressa Food Product ambapo alimuagiza meneja wa Tanesco Mkoa wa Pwani kuhakikisha ndani ya miezi miwili umeme uwe umefika kiwandani hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hawa TANESCO kweli ovyo sana. Hivi kutafuta fursa za biashara kwa ajili ya biashara yao wenyewe ya kuuza umeme na kutafuta wateja wenye uwezo wa kulipa inahitaji maagizo ya Rais? Wale wanaodai shirika hili livunjwe na kugawanywa kampuni za Uzalishaji na Usambazaji wanayo hoja yenye nguvu. Wasipuuzwe.

    ReplyDelete
  2. Inapendeza zaidi kufatana na hadhiye alau kutanguliza neno 'Mh. Rais .....' kuliko hiyo ya moja kwa moja tu Rais Magufuli as if is just a 'layman'. Ni maoni yangu asikereke yeyote.

    ReplyDelete
  3. Yaani Tanesco ni mazombwe na mamburura yaani mpaka Rais aseme ndio wapeleke umeme, wakati ni fursa yao wenyewe ya kibiashara,hao ovyo sana ni shirika la ajabu duniani....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...