Timu ya Tanzania ya kuogelea baada ya kukabidhiwa kombe la CANA kanda ya tatu Kigali, Rwanda wakiwa pamoja na timu ya Zambia washindi wa pili na washindi wa tatu Uganda.

Nchi ya Tanzania imeandika historia katika mchezo wa kuogelea baada ya kuchukua kombe la mashindano ya kuogelea ya CANA kanda ya tatu jijini Kigali katika nchi ya Rwanda siku ya jumapili tarehe 20 Novemba, 2016. 

Timu ya Tanzania imerejea nchini siku ya Jumatatu saa nne na nusu usiku kwa ndege ya Rwanda na kupokelewa na viongozi wa TSA wakiongozwa na Mkurugenzi wa Fedha Philip Saliboko na Mkurugenzi wa Ufundi TSA Amina Mfaume,pamoja na wazazi, waogeleaji na watanzania wengine ambao waliungana kuishangilia timu hiyo ilipowasili kwa nderemo na vifijo katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere.

Tanzania imeweka historia nyingine baada ya kujinyakulia medali 99 kati ya hizo medali ya dhahabu ni 32, Silver 35, na bronze 32 ambapo wachezaji wetu wote 24 walioshiriki mashindano haya na kuleta ushindi wa kihistoriaTanzania wamepata medali.
Balozi wa Tanzania nchini Rwanda Ali Idi Siwa akisalimiana na Mchezaji Joseph Sumari wa Kuogelea.
Kutoka kushoto Kocha msaidizi Grace Sanford, Makamu Mwenyekiti Thauriya Diria, Mheshimiwa Balozi Ali Idi Siwa, Kocha Mkuu Ferick Kalengela na Katibu Mkuu TSA Ramadhan Namkoveka.
Makamu Mwenyekiti wa TSA Thauiriya Diria kushoto, Balozi Ali Idi Siwa katikati na Katibu Mkuu wa TSA Ramadhan Namkoveka wakati walipoenda kumuonyesha kombe Tanzania wamepata wakati wa mashindano ya CANA kanda ya tatu.
Timu ya Tanzania ikiwa na kombe katika ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchin i Rwanda.
Viongozi wa CANA kanda ya tatu wakijadiliana jambo kabla ya kuitangaza Tanzania washindi wapya wa michuano hiyo ya CANA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...