Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
SHIRIKA la Viwango Nchini (TBS) limewatangaza washindi wa shindano la uandikaji wa insha lililoandaliwa na Shirika la Mazingira Duniani (UNEP) lililoshirikisha shule za msingi na sekondari Tanzania nzima.

Akizungumza kabla ya utoaji tuzo hizo,Kaimu mkurugenzi mkuu wa TBS Egid Mubofu amesema hatua hii itasaidia sana kuweza kutoa elimu kwa wananchi hasa baada ya wanafunzi hawa kuonesha jitihada kubwa za kuondokana na suala zima la uchafuzi wa mazingira.



Katika shindano hilo lililoshirikisha takribani wanafunzi 75 kutoka sehemu mbalimbali nchini lilianza rasmi mwezi Septemba na kumalizika mwishoni mwa mwezi Oktoba na kufanikiwa kupatikana kwa washiriki nane kwa shule za Msingi na 10 kutoka shule za Sekondari.



Mshindi wa kwanza kwa upande wa shule ya msingi ilichukuliwa na Nairath Ngururu kutoka shule ya Wasichana Almutanzir huku nafasi ya pili ikiendelea Eldred Medard kutoka shule ya Valentine na nafasi ya tatu kwenda kwa Shiluni Laizer kutoka shule ya Havard zote za Jijini Dar es salaam.

kwa upande wa sekondari,wasichana waliendelea kutamba baada ya Zainab Kambi kutoka Academic Internaational kushika nafasi ya kwanza, Frank Kapinga kutoka Kibaha Sekondari kushika nafasi ya pili na nafasi ya tau kuchukuliwa na Pius Mollel kutoka St Jude
 ya Jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa mradi huo, Mary Meela amesema kuwa washiriki wote ni washindi kwani waliweza kuingia kwenye hatua ya mwisho ya mchujo na wanatakiwa kuja kuwa mabalozi wakubwa katika suala zima la mazingira.

Afisa mwakilishi wa UNEP, Clara Nakenya amesema kuwa hatua hii ni moja ya malengo 12 yaliyofikiwa kwa ajili ya kupambana na masuala ya mazingira kwani insha hizi zina elimu ya kutosha kwa rika zote husuani watoto, vijana na wazee katika kufanya maamuzi kuhusiana na mazingira.
Kaimu mkurugenzi mkuu wa TBS Egid Mubofu akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa shindano hilo walioingia fainali pamoja na majaji wa shindano hilo.
Kaimu mkurugenzi mkuu wa Shirika la Viwango Nchini (TBS) Egid Mubofu akizungumza wakati wa utoaji wa zawadi kwa washindi wa shindano uandishi wa insha wa mazingira lililoratibiwa na Shirika la Mazingira Duniani (UNEP) kushirikiana na shirika hilo.
Afisa mwakilishi wa Shirika la Mazingira Duniani (UNEP), Clara Nakenya akizungumza wakati wa utoaji wa zawadi kwa washindi wa shindano uandishi wa insha wa mazingira lililoratibiwa na Shirika la Mazingira Duniani (UNEP) kushirikiana na shirika hilo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...