Na Daudi Manongi, MAELEZO

Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) imekusanya shilingi bilioni 8.1 katika robo ya kwanza ya mwaka 2016 ikiwa ni zaidi ya shilingi bilioni 1.6 ya robo ya kwanza ya mwaka 2015 ambapo ilipata mapato ya zaidi ya shilingi bilioni 6.5.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Bw.Masanja Kungu Kadogosa wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.

Bwana Masanja anasema kuwa huduma ya usafirishaji abiria imezalisha mapato ya wastani wa shilingi bilioni 1.1 katika kipindi cha mwaka 2016 na Wastani wa shehena kwa robo mwaka imeongezeka na kufikia tani 63,251 ukilinganishwa na tani 48,681 zilizosafirishwa katika kipindi kama hicho mwaka jana.

Aidha kati ya mwezi Juni hadi Octoba mwaka 2016 kampuni imetekeleza miradi midogo kadhaa ya kujenga michepuo ya reli kwenda kwenye viwanda vya wateja wa TRL wenye kuzalisha shehena,ambapo Baadhi ya miradi ya reli za michepuo zilizojengwa ni kwenda kiwanda cha mbolea cha Yara kilichopo Kurasini na kiluwa Group ya Mlandizi huku michepuo mingine inatarajiwa kujengwa kuelekea viwanda vya Saruji vya Rhino na Sungura vilivyopo mkoani Tanga.

Aidha Bw.Kadogosa amesema kuwa wamefanikiwa kufanya ukarabati wa mabehewa ya mizigo 120 yaliyogharimu shilingi milioni 700 na kusema kama yangefanyiwa ukarabati nje ya nchi yangegharimu shilingi bilioni 26.

Mbali na hayo menejimenti ya TRL inaendelea kutoa kipaumbele katika kutatua madai ya wafanyakazi wake ikiwemo kuwasilisha Michango katika mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF),WADU na Saccos NMB ambapo baada ya kuwasilisha makato wafanyakazi wameanza kupata huduma stahiki.

Aidha malimbikizo ya nyongeza ya mshahara yameshatengewa shilingi milioni 600 ambazo zimelipwa ikiwa ni awamu ya tatu na menejimenti inajipanga kumaliza awamu nyingine zilizosalia.

Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa wadau na wananchi kuhakikisha wanalinda miundombinu ya reli na kuripoti mara moja kwenye vyombo vya dola wale wote wanaohujumu miundombinu kwa manufaa binafsi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...