KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) leo imefunga huduma za mawasiliano ya intaneti bure katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) itakayowawezesha madaktari, wafanyakazi wengine, wagonjwa pamoja na wananchi wanaofika katika kituo hicho kupata huduma ya mawasiliano ya intaneti bure yenye kasi ya hali ya juu. 

 Akikabidhi huduma hiyo, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Wazir W. Kindamba alisema kampuni hiyo imetumia jumla ya shilingi milioni 120 kufunga huduma bure ya intaneti katika kituo hicho na itatolewa kwa muda wa mwaka mmoja ikiwa ni kuiwezesha taasisi hiyo kuendesha shughuli zake kwa ufanisi.

 Akifafanua zaidi Bw. Kindamba alisema huduma hiyo ambayo itagharimu shilingi milioni 10 kwa kila mwezi ambazo zitakuwa zikilipwa na TTCL ikiwa ni mchango wake kwa jamii na hasa kwa matibabu yanayofanyika katika kituo hicho itakuwa ikitolewa kwa teknolojia ya Wi-Fi bure kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Novemba 10, 2016 hadi Novemba 10, 2017.

 "Kwa kuzingatia umuhimu wa sekta ya afya na kazi kubwa inayofanywa na Taasisi hii, TTCL tumetoa intaneti yenye kasi hadi kufikia spidi ya 100Mbps, spidi hii itasaidia kuongeza uwajibikaji katika kutoa huduma kwa wananchi, kuimarisha mawasiliano miongoni watumishi wa JKCI na nje ya Taasisi, kupashana habari za kitabibu na kubadilishana taarifa za kitabibu miongoni mwa wataalamu kutoka hospitali za ndani na hospital za nje ya mipaka ya Tanzania," alisema Kindamba. 
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Wazir W. Kindamba (kulia) akimkabidhi kibao cha kuashiria huduma bure ya intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi (kushoto) leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya Kampuni ya TTCL kukabidhi huduma hiyo. Huduma hiyo ina itakayotolewa kwa mwaka mmoja inagharimu shilingi milioni 120.Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Wazir W. Kindamba (kulia) akimkabidhi kibao cha kuashiria huduma bure ya intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo  ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi (kushoto) leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya Kampuni ya TTCL kukabidhi huduma hiyo. Huduma hiyo ina itakayotolewa kwa mwaka mmoja inagharimu shilingi milioni 120.Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Wazir W. Kindamba (kulia) akimkabidhi kibao cha kuashiria huduma bure ya intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi (kushoto) leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya Kampuni ya TTCL kukabidhi huduma hiyo. Huduma hiyo ina itakayotolewa kwa mwaka mmoja inagharimu shilingi milioni 120.Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Wazir W. Kindamba (kulia) akimkabidhi kibao cha kuashiria huduma bure ya intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo  ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi (kushoto) leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya Kampuni ya TTCL kukabidhi huduma hiyo. Huduma hiyo ina itakayotolewa kwa mwaka mmoja inagharimu shilingi milioni 120.Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi akizungumza katika hafla ya Kampuni ya TTCL kukabidhi huduma ya bure ya intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Huduma hiyo itakayotolewa kwa mwaka mmoja inagharimu shilingi milioni 120.Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi akizungumza katika hafla ya Kampuni ya TTCL kukabidhi huduma ya bure ya intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Huduma hiyo itakayotolewa kwa mwaka mmoja inagharimu shilingi milioni 120.Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Wazir W. Kindamba (kulia) akizungumza katika hafla ya kampuni ya TTCL kukabidhi huduma bure ya intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi akifuatilia.   Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Wazir W. Kindamba (kulia) akizungumza katika hafla ya kampuni ya TTCL kukabidhi huduma bure ya intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi akifuatilia. 
Picha ya pamoja mara baada ya zoezi la makabiadhiano. Picha ya pamoja mara baada ya zoezi la makabiadhiano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...