Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii
Katibu mkuu wa Wizara ya habari Sanaa na michezo Profesa Elisante Ole Gabriel amesema kuwa tatizo la ukosefu wa ajira Afrika ni matokeo na sio tatizo kama watu wanavyosema ama dhania.
Profesa Gabriel amesema hayo katika Mdahalo wa wanazuoni kutoka Afrika Mashariki uliofanyika katika ukumbi wa mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
"Tatizo kubwa la Afrika ni soko na kubadilisha fikra za vijana katika bara letu kwa kupata ellimu juu ya namna Watakavyoweza kujikwamua kiuchumi hali itakayosadia kuondokana na umaskini uliokithiri hivyo ifike hatua watu wasiwe wanahitaji kupewa pesa pindi inapohitaji kupewa elimu "amesema Profesa Gabriel
Amewataka wakufunzi wa vyuo kurudi vyuoni na kubadilisha mawazo ya vijana kurudi katika mtazamo chanya wa kujipatia maendeleo kuliko kusubiri kusukumwa na watu juu ya kupata ajira.
Profesa Elisante Ole Gabriel akizungumza katika Mjadala huo
washiriki wakimsikiliza Profesa Ole Gabriel
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...