UMOJA wa Ulaya (EU) na Umoja wa Mataifa (UN) wamejiunga pamoja kuendesha kampeni ya uelewa wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) nchini Tanzania . Aidha kwa pamoja wamezuru miradi iliyofadhiliwa na EU. Wakiwa Mkoani Iringa wamepata nafasi ya kuzungumza na wanachuo 1,000 kutoka vyuo vikuu vya Iringa na Mkwawa kwenye semina iliyoelezea malengo hayo ya dunia ambayo ni sehemu ya ajenda 2030 ya maendeleo endelevu duniani.

 Kampeni hiyo imelenga kuwafanya vijana waelewe malengo 17 ya dunia ambayo kwa sasa yana mwaka mmoja tangu yapitishwe na kuwatanabaisha wajibu wao katika kufanikisha utekelezaji wake ndani ya mazingira ya Tanzania.

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela ripoti na makabrasha mbalimbali ya Umoja wa Mataifa mara baada ya kuhitimisha semina kuhusu SGDs kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa.
Mwongoza wageni katika Makumbusho ya mkoa wa Iringa, Deonis Mgumba akitoa maelezo ya vifaa mbalimbali vilivyokuwa vikitumika enzi za utawala wa kichifu kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) na Katibu Tawala Msaidizi -Miundombinu wa Mkoa wa Iringa, Henry Mditi (katikati) walipotembelea makumbusho hayo mjini Iringa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro wakitwanga mahindi kienyeji katika moja ya kinu kilichokuwa kinatumika enzi hizo za utawala wa kichifu kilichopo katika makumbusho hayo.
Mwongoza wageni katika Makumbusho ya mkoa wa Iringa, Matatizo Kastamu akitoa maelezo ya picha mbalimbali zenye kumbukumbu za utawala wa kichifu na historia ya mji wa Iringa kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro.
Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro (kushoto), Mtalaam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu na Meneja wa Mradi wa Fahari Yetu, Jan Kuever wakipitia vipeperushi vyenye maelezo ya kina ya Mradi wa Fahari Yetu unaoendesha Makumbusho na Kituo cha Utamaduni mkoa wa Iringa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro katika picha ya pamoja kwenye sanamu maalum za mavazi ya kipindi cha utawala wa Chifu Mkwawa walipotembelea Makumbusho ya mkoa wa Iringa.

HABARI ZAIDI SOMA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...