Na. Lilian Lundo – MAELEZO

IMEELEZWA kuwa Uongozi bora na matumizi bora katika usimamizi wa fedha za Serikali ni miongoni mwa sababu zilizoiletea Tanzania maendeleo tangu ilipopata uhuru mwaka 1961.

Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Spika Mstaafu, Pius Msekwa wakati wa mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii kuhusiana na hatua ambazo Tanzania imepiga tangu ipate uhuru mwaka 1961.Msekwa alisema kuwa uongozi bora pamoja matumizi bora ya fedha ndizo nguzo kuu zilizoiletea Tanzania maendeleo yanayoonekana leo ambapo takribani sekta zote zimepiga hatua kubwa ukilinganisha na kipindi cha uhuru mwaka 1961. 

“Wakati tunapata uhuru mwaka 1961 tulirithi vitu vichache kutoka kwa wakoloni ambavyo ni shule hospitali ya Muhimbili iliyokuwa ikijulikana kama Princess Magreth ambayo kwa sasa imepiga hatua na kuweza kufanya upasuaji wa moyo ambao haukuwahi kufanyika kwa miaka ya nyuma,” alifafanua Msekwa.

Alisema kuwa maendeleo yote hayo yametoka na juhudi za marais waliopita na aliyepo, katika uongozi wao ambapo wamekuwa wakipambana na maadui watatu wa maendeleo ambao ni ujinga, maradhi na umasikini.Aidha alisema kuwa viongozi hao wamekuwa wakipambana na maadui hao kulingana na fedha ambazo zimekuwa zikipatikana katika kipindi cha uongozi wao.

Msekwa aliwataka Watanzania kuendelea kumuenzi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kutokana na misingi aliyoiacha ambayo imeweza kutumiwa na viongozi wa nchi na kuendelea kuleta maendeleo ambayo Tanzania inajivunia hadi sasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...