Na Humphrey Shao,
Globu ya Jamii 
 HAKIMU Mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi kisutu, Mhe. Cyprian Mkeha amewataka mawakili wa serikali kuwasilisha ushahidi wa kesi inayomkabili mchungaji  Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima baada ya kushindwa kumfikisha shahidi husika kwa kipindi cha miezi sita. 
Hakimu Mkeha alitoa maamuzi hayo baada ya wakili wa Jamhuri Bi. Jacguline Nyantoli na mwendesha mashtaka kuomba kuahirishwa kwa kesi hiyo ya kutoa lugha ya matusi inayomkabili mchungaji Gwajima kwa kukosekana kwa shahidi mahakamani hapo kwa madai ya kuwapo na kesi nyingi siku hiyo. Mhe, Hakimu alisema hiyo sio hoja ya msingi ya kutokuwepo kwa shahidi huyo kwa kipindi cha miezi sita.  
Katika kesi hiyo ya utoaji wa lugha ya matusi iliyokuwa inamkabili mchungaji Gwajima alikuwa akitetewa na wakili Peter Kibatala ambaye aliridhia maamuzi ya wakili mpaka hapo kesi itakapotajwa tena Desemba 1, 2016.
 Mchungaji Josephat Gwajima akiwa na wakili wake Bw/ Peter KIbatalaa wakitoka Mahakamani
Baadhi ya waumini wa Kanisa la Ufufuo na uzima wakiwa nje ya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...