SERIKALI
kupitia Shirika lake la umeme nchini TANESCO limefanya uwekezaji mkubwa kwenye
miradi mbalimbali ya umeme yenye thamani ya Shilingi Trilioni 5.35, Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika hilo, Mhandisi Felchesmi Mramba amewaambia waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam, leo Novemba 24, 2016.
Akitoa
ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali muhimu ya Shirika hilo, Mhandisi Mramba
alisema, “Katika historia ya sekta ya umeme, haijawahi kutokea uwekezaji mkubwa
kufanyika kwa wakati mmoja kama ilivyo sasa, Miradi yote ya umeme inayoendelea
na ambayo tayari iemtengewa fedha ina thamani ya Shilingi Trilioni 3.85, na
majadiliano kati ya Serikali na Exim Bank ya mradi wa Dar es Salaam-Arusha wa
Shilingi Trilioni 1.5 yakiwa katika hatua za mwisho.” Alifafanua Mhandisi
Mramba.
“
Uwekezaji huu unathibitisha kwamba nia ya Serikali ya awamau ya tano ya
kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda sio ya maneno matupu bali inaambatana na
vitendo kwa uwekezaji madhubuti kwenye umeme.” Alisema.
Mhandisi
Mramba alitaja Miradi hiyo mikubwa ya umeme kuwa ni pamoja na ule wa upanuzi wa
Kinyerezi I, Kinyerezi II, mradi wa Backbone, Kenya-Tanzania, TEDAP,
Makambako-Songea, Uboreshaji umeme jijini Dar es Salaam, City Centre-Dar es
Salaam, Electricity V, Bulyanhulu-Geita, Geita Nyakanazi na Rusumo Power Plant
(T), miradi yote hii ikiwa na jumla ya thamani ya Shilingi Trilioni 3.85.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, (katikati), akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo Novemba 24, 2016. Alikuwa akitoa ufafanuazi kuhusu masuala muhimu ya TANESCO. Wengine pichani, kulia ni Meneja wa Vyuo vya TANESCO, Mhandisi Said Msemo na kushoto ni Kaimu Meneja Uhisano wa Shirika hilo, Leila Muhaji.NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo
Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji, (kushoto), akizunguzma jambo
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...