Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

WAJASIRIAMALI zaidi ya 200 katika Kata ya Bunju jijini Dar es Salaam wamepata mafunzo ya siku 10 katika ujuzi mbalimbali ili kuwasaidia kukuza ujasiriamali na kuongeza kipato katika familia na jamii kwa ujumla. 

Mafunzo hayo yaliendeshwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Kanda ya Dar es Salaam kuanzia tarehe 14 hadi 25,November 2016 chini ya Mpango wa Kukuza Ujasiriamali katika Sekta isiyo Rasmi (INTEP) na yalihusisha stadi za utegenezaji wa Batiki, Mapishi, Mapambo na Ufundi wa Upakaji rangi.

Akizungumza katika hafla ya kufunga Mafunzo hayo siku ya Ijumaa November 25, 2016 Afisa Mtendaji wa Kata ya Bunju Shumasike Shumasike alisema, mafunzo hayo yameongeza fursa ya ajira kwa wananchi wake na kuiomba VETA kuendelea kutoa mafunzo ya namna hiyo zaidi kwani yatawasaidia wananchi wa kawaida kwa kiasi kikubwa.

Alisema, waliopata mafunzo ni watu ambao walikuwa hawana shughuli yeyote ya kuwaingizia kipato hivyo kupata mafunzo yameonyesha njia ya kuweza kuingia katika soko la ajira kwa kuanzisha biashara mbalimbali.

Shumasike aliwaasa wanufaika wa mafunzo kutumia vyema vyeti walivyovipata na kuidhihirishia jamii kuwa ujuzi walioupata ni wa manufaa makubwa kwao na kwa jamii inayowazunguka na sio kurudi katika hali waliyokuwa nayo mwanzo.

Alisema fedha ya ahadi ya Rais iliyotolewa kwa kila mtaa kunufaika na sh. Milioni 50 kwa ajili ya wajasirimali zitatolewa kwa vikundi na sio kwa mtu mmoja mmoja hivyo wajiandae kwa kutengeneza vikundi na kuvisajili ili fedha hizo zitakapowasili waweze kunufaika.

Naye Mkurugenzi wa Kanda ya VETA Dar es Salaam, Habib Bukko alisema anaamini waliopata mafunzo hayo watayatumia ipasavyo katika kubadilisha maisha yao na kwamba VETA inaendelea na juhudi za kuhakikisha mafunzo hayo yanafikia makundi mengi zaidi.

Mmoja ya walionufaika na Mafunzo hayo, Joyce Lweganwa amesema watatumia mafunzo hayo katika kutengeneza kipato na kuitaka VETA kufikia watu wengine kutokana na ukweli kwamba wahitaji wa mafunzo ya aina hiyo ni wengi sana katika jamii.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Bunju Shumasike Shumasike akijionea bidhaa mbalimbali za batiki zilizotengenezwa na wajasiriamali waliopatiwa mafunzo na VETA jijini Dar es Salaam.
.Sehemu ya wajasiriamali waliopata mafunzo ya mapishi wakionesha vyakula mbalimbali walivyoandaa baada ya mafunzo
Wahitimu wa mafunzo ya Upakaji rangi katika picha ya pamoja na Mtendaji wa Kata ya Bunju Shumasike Shumasike wakati wa kufunga mafunzo hayo jijini Dar es Salaam.

Moja ya kazi waliyoifanya wahitimu wa mafunzo ya upambaji waliopata mafunzo kutoka VETA kama bwana harusi na Bibi harusi .

Afisa Mtendaji wa Kata ya Bunju katika picha ya pamoja na wajasiriamali waliopata mafunzo ya utengenezaji batiki yaliyotolewa na VETA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...