VIJANA wa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani wamesema kuwa kitendo cha Mbunge wa Jimbo hilo Abdallah Ulega kupiga marufuku kukodi wachezaji Kutoka Nje ya Wilaya hiyo imeleta changamoto kwao kuonesha vipaji vyao Kwenye ligi ya mbunge inayoendelea.

Wamesema kuwa wao kama vijana ndio wakati muafaka kwao kuonesha vipaji vyao na uwezo ili mwisho wa siku wapate nafasi ya kushiriki Kwenye ligi mbalimbali.Mbunge Ulega ameazisha Ligi ya mbunge ambapo hivi sasa timu Kutoka kila kijiji zinapambana na baadae zitatoa timu moja ya Kata ambayo itakwenda kushindana na Kata zingine zilizopo ndani ya Wilaya ya Mkuranga.

Akizungumzia ligi hiyo jana wilayani humo Kijana khatibu Dadi alisema kuwa mbunge Ulega amedhamiria kuinua vipaji vya vijana wa Mkuranga na hiyo nikutokana na wito wake wakutaka ligi hiyo ishirikishe vijana wa maeneo husika tofauti na wanavyofanya kungineko.

"Kwa kifupi kila mtu anampongeza Mh.Mbunge Kwa uamuzi wake kwani lazima ifike wakati sisi kama vijana wa Mkuranga tuoneshe wenyewe uwezo na vipaji vyetu na tunaamini kupitia ligi hii ya Mbunge tutapata timu kabambe ya Wilaya."alisema Dadi
 Katibu wa mbunge wa Mkuranga Bw Omar Kisatu akipeana mikono na baadhi ya wachezaji wa timu shiriki mashindano ya Ulega Cup yanayoendelea kutimua vumbi Wilayani Mkuranga.

 Diwani wa Kata ya Panzua Bw Juma Magaila akiongea na waandishi wa habari kuhusu ligi ya Ulega Cup  inayoendelea  Wilayani Mkuranga.
Katibu wa mbunge wa mkuranga Bw Omar Kisatu Akiongea na waandishi wa habari kuhusu mashindano hayo ya Ulega Cup yanayoendelea kutimua vumbi Wilayani Mkuranga.
 Diwani wa Kata ya Mkamba Wilayani Mkuranga Bw Hassan Dunda Akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na Mtiririko mzima wa ligi ya Ulega Cup unaondelea huko Wilayani Mkuranga.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...