Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii

YALI Regional Leadership Centre ya Nchini imedhamiria kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana Tanzania Bara na Visiwani kwa kumualika moja ya waandamizi wa masuala ya ujasiriamali kutoka nchini Jordan Laith Al Qassam ili kutoa mafunzo mbalimbali kwa kuhakikisha wanapata nafasi za kujiajiri na kuongeza pato la taifa.

Akizugumza kabla ya kuanza semina hiyo,MuĂ ndaaji wa Semina hiyo Fabian Shayo amesema kuwa mafunzo hayo yajulikanayo kama Blue Ocean Strategy yatahusisha zaidi masuala ya ujasiriamali hususani kwa vijana na mkufunzi Al Qassama ambaye amebobea katika masuala hayo atatoa elimu kwa vijana waliojitokeza.

Shayo amesema Blue Ocean Strategy imeweza kusaidia watu wengi hususani vijana katika masuala ya ujasiriamali na hata kuanzisha makampuni duniani kote pia imeweza kutengeneza soko la kibiashafa na kukuza faida.

Mkufunzi wa mafunzo hayo, Al Qassama ambaye ni mmoja ya waandamizi wa kiwanda cha Jordan ICT na kukiwezesha kuwa moja ya makampuni makubwa duniani amesena kuwa vijana wengi wanaamini kuwa fedha ndiyo kila kitu na kushindwa kuelewa kuwa mawazo yanaweza kuwa msaada kwao.

Blue Ocean Strategy itaendeshwa katika vipindi vitatu tofauti kwa bara na visiwani kwa ajili ya kuwapatia elimu vijana kwa watakaoleta mabadiliko na maendeleo kwenye sekta ya ujasiriamali kupata fursa za ajira na kukuza kiwango cha maendeleo ya kiuchumi katika taifa.

Katika ukanda wa Afrika Mashariki, Vijana waliowahi kushiriki semina hiyo(Alumni) wametumia fursa hii kuwasaidia vijana wenzao ili kuweza kuangalia wanakwamuka vipi kiuchumi kwa kupitia njia ya ujasiriamali.
Mwenyekiti wa kamati ya uandaaji wa mafunzo hayo, Fabian Shayo akizungumza na waandishi wa habari juu ya mikakati yao ya kusaidia vijana kujikwamua kiuchumi kwa kutumia sera ya ujasiriamali. Kulia ni Mkufunzi Laith Al Qassam na kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya fedha Fortunatus Eklklesiah.
Mkufunzi Laith Al Qassam akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mafunzo hayo ya ujasiriamali kwa vijana na nini wanatakiwa kufanya ili kuondoa dhana ya kuajiriwa au kuamini fedha zinaweza kufanya kila kitu. Kulia ni Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano, Khalila Mbowe na kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya uandaaji wa mafunzo hayo, Fabian Shayo.
Mkufunzi wa Semina hiyo Laith Al Qassam akitoa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana waliojitokeza yaliyoendeshwa na YALI Regional Leadership Centre kwa ukanda wa Afrika Mashariki. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...