Baraza la Wauguzi na Wajunga nchini wametakiwa kutowaonea aibu wale wote wanaoanzisha vyuo vya afya kama mradi wa kujiingizia fedha bila ya kuwa na taaluma hiyo kwani kunapelekea kuhatarisha Maisha na afya za watanzania.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akiweka jiwe la msingi katika jengo la kituo cha kuendeleza wauguzi na wakunga kitaaluma nchini lililopo mjini kibaha Pwani.

“Hatusemi wasianzishe vyuo,bali vyuo vyote viwe vyenye hadhi ya kutoa wataalam stahili ,visajiliwe na vikaguliwe mara kwa mara ili vizalishe wauguzi wenye sifa na ujuzi stahili,uuguzi siyo ujasiliamali,hakikisheni mnavifungia vyuo vyote feki ili tuweze kudhibiti utitiri huu” alisema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy alisema hivi sasa kumekuwepo na utitiri wa vyuo vingi vya uuguzi ambavyo havijasajiliwa na havizalishi wauguzi ambao wanastahili kuajiriwa kwenye sekta ya afya na hivyo kuhakikisha wanasimamia taaluma hiyo na kuvifungia mara moja vyuo vilivyokosa sifa.
Waziri Ummy alisema kuwa serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa unaofanywa na wauguzi katika hospitali zote nchini hivyo maboresho yatafanyika na kuhakikisha upatikanaji wa vitendea kazi kwa wauguzi.

“Asilimia 80 za kazi zote katika hospitali zetu nchini zinafanywa na wauguzi na wakunga hivyo Serikali imesikia kilio chenu na tutahakikisha tatizo hili tunalitatua” alisema Ummy.Hata hivyo Waziri Ummy aliwataka wauguzi kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia maadili na viapo vyao vya kitaaluma kwa maendeleo ya Afya nchini.

Kwa upande wa Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga nchini Bi. Lena Mfalila alisema jengo hilo linajengwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza limegharimu pesa ya kitanzania shilingi bilioni 2.2.Aidha Bi. Mfalila alisema kuwa ujenzi wa kituo hicho ulianza Desemba 2015 kwa awamu ya kwanza na kiinatarajiwa kukamililika na kuanza matumizi yake Januari2017 .
Waziri wa Afya, Maeendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katikati akiweka udongo kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika jengo la kituo cha kuendeleza wauguzi na wakunga kitaaluma nchini lililopo wilayani Kibaha leo Mkoa wa Pwani.

Waziri wa Afya, Maeendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiangalia michoro ya jengo litakavyokua pindi litakapomalizika wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika jengo la kituo cha kuendeleza wauguzi na wakunga kitaaluma nchini lililopo wilayani Kibaha leo Mkoa wa Pwani.
Wenyeviti wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Afya, Maeendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy  Mwalimu hayupo pichani wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika jengo la kituo cha kuendeleza wauguzi na wakunga kitaaluma nchini lililopo wilayani Kibaha leo Mkoa wa Pwani.
Wauguzi mbalimbali wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Afya, Maeendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu hayupo pichani wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika jengo la kituo cha kuendeleza wauguzi na wakunga kitaaluma nchini lililopo wilayani Kibaha leo Mkoa wa Pwani.
Habari/Picha Na Ally Daud.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...