Emmanuel Cornel Matema mwenye umri wa miaka 38 wa Tabata, jijini Dar es Salaam na Mkazi wa Tabora, Ramon Hamisi Mane (22) wamefanikiwa kujishindia kila mmoja kiasi cha Sh milioni 23 baada ya kubashiri vyema matokeo ya mechi mbalimbali za ligi za Ulaya kupitia Kampuni ya m-Bet.
Washindi wote hao, wamekabidhiwa vitita vyao katika hafla fupi iliyofanyika ofisi za m-Bet, jijini Dar es Salaam leo Jumatano Novemba 30, 2016 chini ya usimamizi wa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abbas Tarimba. 
Akizungumza katika hafla hiyo, Tarimba aliwapongeza washindi hao na kuwataka kuhakikisha wanazitumia vema fedha hizo ili ziweze kusawasaidia katika kuboresha maisha yao. 
“Nichukue fursa hii kuwapongeza m-Bet kwa kuendesha bahati nasibu hii ambayo imeonekana kuwanufaisha Watanzania wengi waliojishindia mamilioni ya shilingi hadi sasa. Lakini pia nitoe rai kwa washindi kuhakikisha wanazitumia ipasavypo fedha wanazoshinda ili ziweze kuboresha maisha yao na si vinginevyo, ukizingatia kwa sasa maisha ni magumu sana,” alisema Tarimba.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa m-Bet, Dhiresh Kabba, alisema kuwa wawili hao walifanikiwa kuzoa kitita hicho baada ya kufanikiwa kutabiri matokeo ya mechi 15 za ligi za Ulaya.
“Tunafarijika kuwakabidhi Matema na Mane kitita chao kiasi cha Sh milioni 23 ambapo watagawana sawa sawa,” alisema Kabba.
Aliwataka watanzania kuchangamkia kutumia mtandao wa intaneti kuonyesha ushabiki halisi wa soka akisema kuwa Perfect 12 ni mchezo wa ziada unaoruhusu kutabiri mechi 12 kwa Tsh 1,000 tu ambapo ukipatia zote  unaondoka na kitita chako mchana kweupe. 
Akielezea furaha yake kwa kushinda fedha hizo, Matema ambaye ni mjasiriamjali, alisema: “Nawashukuru sana m-Bet kwa kuniwezesha kushinda fedha hizi ambazo nitazitumia kuongeza mtaji wa biashara zangu na mahitaji binafsi.” 
Naye Mane ambaye ni mwanafunzi na mjasiriamali, alisema: “Fedha hizi zitanisaidia sana katika biashara zangu, lakini zaidi ikiwa ni masomo kwani nimekuwa katika wakati mgumu linapokuja suala la ada na mahitaji mengineyo ya shule. Ahsante sana m-Bet.” 
Kuhusu m-Bet, ni Kampuni iliyosajiliwa chini ya Sheria za Tanzania na kupewa leseni na Bodi ya Michezo ya kubahatisha tanzania kwa lengo la kufanya upatikanaji rahisi na mwingiliano wa huduma ya mchezo wa kubahatisha (Sim Betting) nchi nzima.
“Kushiriki, ingia www.m-bet.co.tz, chagua kucheza kawaida au Perfect 12 ambapo kwa Shilingi 1000, unachagua matokeo 12. Ukipata yote sawa, unanyakua kikapu cha m-Bet,” alisema Kaba
 Washindi wa M-bet,Emmanuel  Katema (kushoto) na Ramon  Mane wakifurahia zawadi yao  wakati walipokabikdhiwa hundi ya mfano ya Sh.Milioni Arobaini na sita (46,000,000) baada ya kuibuka washindi wa Perfect 12. Makabidhiano hayo yalifanyika jijini Dar es Salaam leo Novemba 30, 2016

 Kaimu Mkurugenzi wa  Uendedshaji na Sheria wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, James Mbalwe akiwakabidhi hundi ya mfano wa Sh. Milioni Arobani na sita (46,000,000/=) , wa washindi  wa M-bet, Ramon  Mane (kulia) na  Emmanuel  Katema (wa pili kulia), ambao waliibuka  washindi  wa Perfect 12. Makabidhiano hayo jijini Dar es Salaam leo Novemba 30 yalihudhuriwa na Mkurugenzi wa M-bet, Dhiresh Kaba ( wa pili kushoto).
Mkurugenzi wa M-bet, Dhiresh Kaba (katikati) akiungana na washikndi wa M-bet, Emmanuel  Katema (kushoto) na Ramon  Mane, kushangilia mara baada ya makabidhiano ya mfano wa hundi wa Sh. Milioni Arobaini na Sita kwa wahindi hao walioibuka kidedea wa  Perfect 12.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...