WAKULIMA wa korosho Wilaya ya Tunduru, wameondokana na umasikini
kutokana na kupata soko la uhakika baada ya Kampuni ya Namela General
Trade kushinda zabuni ya kununua zao hilo wakulima kwa bei ya Sh 3,757
kwa kilo, ikizishinda kampuni nyingine saba.
Hadi kufikia Novemba 14, kulikuwa na zaidi ya tani 541 zilizoingizwa
katika ghala la Chama Kikuu cha Ushirika Wilaya ya Tunduru (Tancu)
ambako kampuni hiyo ilipewa kununua korosho tani 400 huku Kampuni ya
Machinga iliyoshinda nafasi ya pili katika mnada huo, ikipata kibali cha
kununua tani 141 kwa bei ya Sh 3,750.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...