Wanafunzi wawili wa shule ya Academic International ya Tanzania wameweka historia katika mitihani ya mtahala wa Cambridge baada ya kushinda nafasi ya kwanza duniani katika masomo ya hisabati na kompyuta.

Wanafunzi hao ni Harshvardhan Babla aliyekuwa wa kwanza katika mtihani wa somo la kompyuta kwa wanafunzi wa kidato cha tano Abishek Sankaranarayanan aliyeshinda nafasi ya kwanza katika mtihani wa hisabati kwa wanafunzi wa kidato cha nne.

Wanafunzi hao walikabidhiwa vikombe na vyeti na mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni wa India, Inder Jit Sagar. Pia walimu wa masomo hayo, Thadei Mwinuka ambaye anafundisha somo la kompyuta na Walter Mlowe wa somo la hisabati nao walikabidhiwa vyeti vya pongezi kwa kufanya vizuri.

Akizungumza katika halfa maalum ya kuwapongeza wanafunzi hao na walimu wa masomo hayo, Mkuu wa shule hiyo, Shyama Santhosh alisema kuwa wamefarijika na ushindi huo ambao umeiletea sifa shule, walimu nan chi kwa ujumla.

“Huu ni ushindi mkubwa kwa shule, walimu nan chi kwa ujumla, mtihani wa Cambridge unafanywa na maelfu ya shule duniani na shule yetu imeibuka katika nafasi ya kwanza kwa masomo hayo mawili, ni jambo la kujivunia sana, hii inaonyesha kuwa walimu wetu wapo makini katika kufundisha,” alisema Santhosh.

Mkurugenzi wa shule hiyo, Yusuf Kalindaga amesema kuwa wanajivunia kwa matokeo hao mazuri ambayo yamewafanya kuwa shule pekee Tanzania kushika nafasi hizo za kwanza.
Wanafunzi wa shule ya Academic International school, Harshvardhan Kabla (kushoto) ambaye ameshika nafasi ya kwanza duniani katika somo la Kompyuta kwa wanafunzi wa “A Level” kwa mitihani ya Cambridge na Abishek Sankaranarayanan(kulia) ambaye ameshinda nafasi ya kwanza kwa somo la hisabati kwa mitihani ya Cambridge kwa wanafunzi wa kidato cha nne wakiwa katika picha ya pamoja katika sherehe maalum ya kuwapongeza.
Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni wa India, Inder Jit Sagar akimkabidhi cheti na kombe mwanafunzi wa Shule ya Academic International, Harshvardhan Kabla (kulia) kwa kushinda nafasi ya kwanza duniani katika somo la Kompyuta kwa wanafunzi wa “A Level” kwa shule zinazofuata mtahala wa Cambridge.
Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni wa India, Inder Jit Sagar akimkabidhi cheti na kombe mwanafunzi wa Shule ya Academic International, Abishek Sankaranarayanan(kulia) kwa kushinda nafasi ya kwanza duniani katika somo la Hisabati kwa wanafunzi wa “O Level” kwa shule zinazofuata mtahala wa Cambridge.
Baadhi ya wazazi na wanafunzi wa shule ya Academic International wakiwa katika hafla hiyo .



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...