Na George Binagi-GB Pazzo.

Wanatasinia ya Filamu mkoani Geita wamepewa mtihami ambao hata hivyo ni mwepesi ikiwa watakuwa na dhamira ya dhati ya kuikuza tasnia hiyo. 

Mtihani huo umetolewa hii leo na Waziri wa Afya Zanziar, Mahmood Kombo, aliyekuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, kwenye kikao baina ya wasanii wa filamu mkoani Geita na Bodi ya Filamu nchini.

Mtihani wenyewe ni wanatasnia hao kwa kushirikiana na chama cha Waigizaji mkoa wa Geita, kuandaa Tamasha la Filamu mkoani Geita ambalo litasaidia kuinua tasnia hiyo mkoani humo, Kanda ya Ziwa na hata nchini kwa ujumla."Mkitayarisha Tamasha lenu, mimi mwakani nitakuja pamoja na familia yangu". Amesisitiza Waziri Kombo akitolea mfano Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar namna linavyofana na kuwatangaza wasanii pamoja na kuwaongezea kipato.

Hata hivyo wanatasnia ya filamu mkoani Geita kwenye risala yao wamesema wanahitaji kupewa mafunzo zaidi juu ya namna ya kuboresha filamu zao pamoja na upatikanaji wa stemp/stika kwa ajili ya ulinzi wa kazi hizo hivyo bodi ya filamu nchini iwasaidie katika hilo ambapo Katibu Mtendaji wa bodi hiyo, Joyce Fesso, amekubalina na maombi yao na kuahidi kufikisha mafunzo ya filamu mkoani Geita kama ilivyokuwa hivi karibuni mkoani Mwanza.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi.Joyce Fesso (kushoto), akizungumza kwenye kikao cha Wanatasnia ya Filamu mkoani Geita hii leo kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Geita.

Mgeni Rasmi alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nhauye, aliyewakilishwa na Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe.Mahmood Thabith Kombo (wa piAli kushoto).

Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti Chama cha Waigizaji mkoani Geita, Rosemary Michael na anayefuata ni Herman Matemu ambaye ni Kaimu Afisa Tawala mkoa wa Geita.
Na BMG
Baadhi ya wanatasnia ya Filamu mkoani Geita waliohudhuria kikao baina yao na Bodi ya Filamu mkoani humo, wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi.Joyce Fesso, ambapo amewasisitiza kuungana pamoja na kutengeneza filamu moja iliyo bora kwa ajili ya kuwatambulisha kwenye soko la filamu na pia kuutambulisha mkoa wa Geita badala ya kuwa na filamu nyingi zisizo na ubora.
Kutoka kulia ni mgeni rasmi, Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe.Mahmood Thabith Kombo ambaye amemwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nhauye.Wanaofuata ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fessoo, Mwakilishi wa balozi wa Tanzania nchini Denmark, Dotto Kahindi pamoja na Mratibu wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (Zanzibar International Film Festival), Robert Manondolo.
Mgeni rasmi kwenye kikao baina ya Bodi ya Filamu nchini na Wanatasnia ya Filamu mkoani Geita, Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe.Mahmood Thabith Kombo (katikati) ambaye amemwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nhauye, akisisitiza wasanii mkoani Geita kushikamana na kushirikiana na viongozi wao pamoja na Serikali na kuandaa Tamasha la Filamu kwa kuwa fursa hiyo wanayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...