Uharibu wa vyanzo vya maji.
 
Na Rhoda Ezekiel  Globu ya Jamii-Kigoma,

MWENYEKITI wa Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe,Elisha Bagwenya amemuomba Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buhigwe kushirikiana na watendaji wake kuunda sheria ndogo ndogo zitakazo toa adhabu kwa baadhi ya wananchi wanao haribu vyanzo vya Maji kwa kufanya shughuli za kibinadam katika vyanzo hivyo hali inayo pelekea Halmashauri kukosa maji.

Rai hiyo aliitoa Jana katika kikao cha Baraza La madiwani wa Halmashauri hiyo Bagwenya alisema kumekuwa na Uhalibifu mkubwa katika vyanzo vya Maji unao sababishwa na wananchi wanaofanya shughuli zao katika vyanzo hivyo na kusababisha uchafuzi wa Maji na kupelekea wananchi kupata magonjwa ya mlipuko ikiwa ni pamoja na kipindu pindu.

Alisema Mkurugenzi kwa kushirikiana na wataaramu kuunda sheria ndogo ndogo za uhifadhi wa misitu na mazingira ziletwe kwenye kikao zijadiliwe na zipitidhwe na Halmashauri ilizianze kutumika na kusaidia vyanzo vya Maji kutunzwa na kuisaidia wananchi kupata Maji safi na Salama.

Hata hivyo Bagwenya alimuomba Muhandisi wa Maji Wilaya kuhakikisha wananweka dawa katika vyanzo vya Maji ilikuhakikisha wananchi na ambapo ya Maji yaliyo safi na Salama na kuweza kuepuka Magonjwa ya mlipuko yaliyo kuwa yakijitokeza kwa kipindi cha nyuma.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe kanali Marko Gaguti alisema Serikali ya wilaya imeandaa Mpango wa kupitankatika kila kijiji kutoa maelekezo kuw Wananchi wote kufanya shughuli zao nje ya mita 60 kutoka katika vyanzo vya maji ilkuweza kulinda vyanzo hivyo na wananchi waweze kupata Maji ya kutosha.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...