Na Dotto Mwaibale
WASAIDIZI
wa kisheria wanawake kutoka Shirika la Equality for Growth (EfG),
wamemuunga mkono Rais Dk. John Magufuli katika uhimizaji wa kufanya
usafi Soko la Temeke Sterio jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
katika tukio hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki sokoni hapo Ofisa
Ufuatiliaji na Tathmini wa EFG, Shaban Rulimbiye alisema wameamua
kufanya usafi wa mazingira katika masoko sita yaliyopo chini ya mradi wa
kupinga ukatili wa kijinsia masoko unaoendeshwa na shirika hilo.
"Tunamuunga
mkono rais wetu kwa jitihada zake anazozifanya za kuhimiza usafi ndio
maana wasaidizi wetu wa kisheria kutoka katika masoko hayo tupo nao hapa
Temeke kufanya usafi na baada ya hapo watatoa elimu kwa wafanyabiashara
ya kupinga ukatili huo " alisema Rulimbiye.
Alisema
ukatili wa kijinsia masokoni si kumshika maungoni mfanyabiasha na
matusi hata pale wanawake wanapofanya biashara zao kwa kuziweka chini
bila ya kuwa katika mazingira mazuri pia ni ukatili wa kijinsia.
Alisema
mpango huo wa kufanya usafi katika masoko hayo ni endelevu na kuwa kila
Jumamosi watakuwa wakifanya hivyo kumuunga mkono rais.
Rulimbiye
aliyataja masoko ambayo yapo chini ya mradi huo ambayo yatanufaika na
usafi huo wa mazingira kuwa ni Temeke Stereo, Mchikichini, Kisutu, Feri,
Gezaulole na Tabata Muslim.
Makamu
Mwenyekiti wa soko la Temeke Sterio, Issa Ndilima alilishukuru shirika
hilo kwa mpango huo wa usafi kwani umeleta hamasa kwa wafanyabiashara wa
soko hasa katika mafunzo wanayopata kupitia wasaidizi wa kisheria
kupinga ukati wa kijinsia masokoni.
Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Shaban Rulimbiye (kushoto), akiwaongoza kufanya usafi Soko la Temeke Sterio Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliwa ni kuunga mkono jitihada za Rais Dk.John Magufuli katika suala zima la usafi wa mazingira.
Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Shaban Rulimbiye (kushoto), akiwaongoza kufanya usafi Soko la Temeke Sterio Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliwa ni kuunga mkono jitihada za Rais Dk.John Magufuli katika suala zima la usafi wa mazingira.
Mifagio ikipigishwa kwata ya usafi.
Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Shaban Rulimbiye (kushoto) na Charles Beatus wakifanya usafi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...