Mwanadiaspora Abraham Sangiwa wa Uingereza  akizungumzia swala la umiliki wa Ardhi nchini kwa wanaDiaspora.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Asante mtoa mada kwa ufafanuzi wa hili sakata. Nafikiri Wantanzania wengi tuliopo nje tunafahamu kwamba kauli ya Lukuvi inasimamia sheria zilizopo sasa. Isipokuwa kinachosukitisha wengi wetu ni maudhui na ya kauli yenyewe kama ukiiangalia na ile clip. Lukuvi anaonekana kabisa anachuki na watu wa nje na lugha aliyotumia sio ya busara hata kidogo. kwa kumnukuu tuu, Lukuvi alisema "kuna watu wamejilipua huko nje...na sasa wanajifanya kuishi hapa kama Watanzania, hawaruhusiwi kumiliki ardhi...[ ]..." Watu anaowazungumzia Lukuvi wanaweza kweli wakawa sio raia wa Tanzania kwa mujibu wa sheria zilizopitwa na wakati na za kibaguzi, lakini pamoja na hilo watu hao bado ni Watanzania kwa maana ya utaifa wao, na si busara wala haki kuwatenga. Kauli kama hizi kutoka kwa viongozi zinaonyesha dhahiri kwamba suala la kubadilisha sheria linakwamishwa na viongozi wenyewe kwenye serikali ya sasa, na ndio maana linaendelea kuwa gumu na "Katiba pendekezwa" pia imewekwa kapuni. Hivyo basi, cha kufanyika hapa ni kama mtoa mada alivyosema kwamba diaspora tuungane pamoja na kuweka itikadi zetu za vyama pembeni, ili kuhakikisha sheria za Tanzania zinalinda haki zetu za msingi, iwe kupitia katiba pendekezwa au amendment ya katiba na sheria za sasa. Uzoefu wangu katika hili unanionyesha kwamba hata diaspora wenyewe tumegawanyika sana katika kupigania haki zetu, na unafiki umekuwa mwingi sana ndani ya jumuiya zinazojiita za Watanzania huko nje. Tubadilikeni,na tuweke maslahi ya wanadiaspora na ya nchi yetu Tanzania mbele, na hili suala litapatiwa ufumbuzi mzuri tu. Mh.Michuzi na wasaidizi wako naomba usibanie ujumbe huu,kwani sijamtukana mtu wala "sijachafua hali ya hewa", hivyo approve the message tafadhali.....

    ReplyDelete
    Replies
    1. Please mchangia mada usikwazike na lugha ya Lukuvi that is so petty. Sheria ndo imempa jeuri ya kuongea hivyo fact ni fact. Hata mimi nimeguswa but lets be matured in dealing with this.

      Delete
  2. Ujumbe maridhawa na ufafanuzi wa kina japo si "wakisheria" unapaswa kuungwa mkono na sote wanadiaspora.

    Tatizo letu wanadiaspora ni kuwa na agenda moja tu - uraia pacha (We seem to be a single agenda constituent). Kwa kweli kuna njia nyingi mbadala za kuhakikisha 'uasilia' wa wale 'walioukana' uraia unatambulika, na si yote yanayotegemea 'uwepo wa uraia pacha.

    Nakubaliana na alivyosema bw Sangiwa kuwa sheria kama ilivyo haina utata kwa sasa. Kilichopo ni kwa jumuia kwa pamoja kujenga hoja yenye mshiko wa kina. Kulalama tu hakusaidii kitu kamwe. Jumuia inabidi iwe pamoja katika hili kwani uasilia hauondoki kwa 'karatasi' kinachoondoka ni 'uraia' tu. Bado tunajivunia 'uasilia' wetu na tutaendelea kujivunia, sisi na vizazi vyetu vijavyo.

    Mwalimu Nyerere alisema "Inawezekana, timiza wajibu wako." Niwakati wa daispora kufanya kwa vitendo.

    ReplyDelete
  3. Mhe lukuvi ameongea hata sidhani kama anajua kweli sheria ya umiliki ardhi Tanzania. Kwa mujibu wa sheria zetu hakuna mtanzania yoyote anayeweza kumiliki ardhi Tanzania, hiyo ipo kwenye constitution. Sasa anaposema watu walio nje hawaruhusiwi kumiliki ardhi ameitoa wapi? Wewe kama mtanzania unayejiita umemiliki ardhi naenda basi kwenye title deed yako usome inasemaje. Kila mtu Tanzania anaomba kibali cha kutumia ardhi kwa miaka 99 halafu ikiisha inabidi uombe tena. Sasa kama serikali ikikataa maombi yako inabidi uwarudishie ardhi yao. Kasome constitution ndio utajua.

    ReplyDelete
  4. Salaam KAka Michuzi,

    Pia ifahamike kwamba aliekutana urai wa TAnzania siku akiwaudhi wenye nchi alikojibanza LAZMA ARUDISHWE NCHINI MWAKE ALIPOZALIWA AU NCHI YA URAIA ALIPOUKANA!

    Mathalan, Fulani ni Mtanzania, akaukana uraia wa Kitanzania na kupewa wa nchi nyignie na wakati anajaza pale anaandika kabisa uraia wake kwa kuzaliwa na Mtanzania!

    Mtu huyu kesho akifanya makosa ya kunyang'anywa uraia wa nchi iel ATARUDISHWA NCHI GANI KAMA SI TANZANIA???

    Je watamkataaa??? kwaini asiruhusiwe kujenga ili bahati mbaya kama hii ikitokea kibanda chake si kitamsadiai??

    inabidi nyie ndugu zetu muungane pamoja kwa hili kwa maslahi yenu wote na wazazi wenu na ndugu zenu maana jinsi ilivo mnaweza hata siku kwenda kuomba Visa ya kuingili nchini mwenu kuja kuwaona wazazi wenu mkakataliwa! Tanzania Sheria inabidi zitizamwe upya

    na si ya kumili ardhi tu bali kuna sharia nyingi sana zimepitwa na wakati, tupo miaka ya 2016 bado kuna baadhi ya sharia za miaka khamsini kweusi! Daaah! TUTAFIKA KWELI TUNAPOKWENDA NAMNA HII?

    ReplyDelete
  5. Tanzania Tanzania. Tunakwenda wapi.... Tunajaribu vitu tusivyoviweza. Ni harari sana hizi kauli.. Haya ngoja tuone tunapokwenda... inaogopesha sana jinsi chuki inavyoanza kuapandikizwa ndani ya taifa lililokuwa na amani kwa miaka mingi. Ni lazima serikali iwe makini sana.

    ReplyDelete
  6. Lukuvi ana wivu tu sisi tunataka kujenga nchi yeye anaturidisha nyuma...magufuli tumbua jipu hilo lipo wazi kabisa kurudisha nyuma maendeleo

    ReplyDelete
  7. The law in Tanzania in the hands of politician we don't know the right and wrong

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...