Na Ally Daud-MAELEZO-MOROGORO 

WATUMISHI wa Umma wametakiwa kufanya mazoezi ya viungo Mara moja kwa wiki ili kujiepusha na magonjwa yasioambukiza ili kujenga watumishi wenye afya imara kwa maendeleo ya taifa.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa magonjwa yasioambukiza (NCD) Prof. Ayoub Magimba wakati Wa kufunga mkutano Wa siku tatu Wa Madaktari na wadau Wa afya ngazi ya mkoa na wilaya katika kupata mpango mkakati wa kujikinga na magonjwa yasioambukiza uliofanyika mkoani Morogoro.

“Katika mkutano huu wa kupata mpango mkakati wa kujikinga na magonjwa yasioambukiza tumeazimia kua na Sera inayoelekeza watumishi wote wa Umma wafanye mazoezi ya viungo siku moja kwa wiki ikiwa ni sehemu ya majukumu yao” alisema Prof. Magimba

Aidha Prof. Magimba amesema kuwa mazoezi hayo ni sehemu ya majukumu ya watumishi wa Umma ili kuwasaidia wale wanaokosa muda wa kufanya mazoezi majumbani kwao ili kujikinga na magonjwa hayo.

Mbali na hayo Prof. Magimba amesema kuwa watanzania wanatakiwa kuepuka matumizi ya Mara kwa mara ya Sigara na vileo kwa pamoja na badala yake wajikite kwenye mazoezi na utumiaji wa vyakula asilia. Kwa upande wake Daktari bingwa Wa magonjwa ya ndani Dkt. Meshack Shimwela ambaye ni mshiriki wa mkutano huo amesema kuwa watanzania wanatakiwa kuzingatia na utekelezaji wa Sheria za barabarani ili kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na ajali mpaka kufikia mwaka 2030.

“Watanzania hasa madereva wa vyombo vya moto wanatakiwa kuzingatia na kutii Sheria za barabarani hususani kuacha kuendesha vyombo vyao wakati wamelewa ili kupunguza asilimia 50 ya vifo vitokanavyo na ajali za barabarani hadi kufikia 2030” alisema Dkt. Shimwela Aidha Dkt. Shimwela amesema kuwa katika mkutano huo wameadhimia kuishauri serikali kutenga maeneo maalum ya kuvutia Sigara pamoja na kuweka muda maalumu wa kunywa pombe ili kujikinga na kuepuka magonjwa hayo.

Mkutano huo uliokutanisha madaktari wa ngazi za mkoa na wilaya zote nchini umelenga kutengeneza Sera na mikakati ya mwaka 2017 hadi 2020 katika kupambana na magonjwa yasioambukiza kama kisukari, kansa,shinikizo la damu, ajali za barabarani na uzito kuzidi kiasi ili kujenga taifa lenye afya na Maendeleo.
Mkurugenzi Msaidizi wa magonjwa yasioambukiza (NCD) Prof. Ayoub Magimba akisisitiza jambo mbele ya madaktari na wadau wa afya ngazi ya mkoa na wilaya hawapo pichani wakati wa kufunga mkutano Wa siku tatu Wa Madaktari na wadau Wa afya ngazi ya mkoa na wilaya katika kupata mpango mkakati wa kujikinga na magonjwa yasioambukiza uliofanyika mkoani Morogoro. 
Baadhi ya Madaktari na wadau wa afya ngazi ya mkoa na wilaya hawapo waklijadili sera na mipango wakati wa kufunga mkutano Wa siku tatu Wa Madaktari na wadau Wa afya ngazi ya mkoa na wilaya katika kupata mpango mkakati wa kujikinga na magonjwa yasioambukiza uliofanyika mkoani Morogoro. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ili upate faida ya mazoezi,inabdi ufanye mazoezi kwa dakika thelathini kila siku, mara TANO kwa wiki. Kufanya mazoezi mara moja kwa wiki ni sawa na sisimizi kutekenya sikio la TEMBO.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...