Frank Mvungi-Maelezo

Serikali imewataka watumishi wa umma kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma ili kuleta ustawi kwa wananchi kwa kutekeleza mipango inayolenga kukuza uchumi na kutoa huduma bora.Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam na Katibu Msaidizi kutoka Ofisi ya Rais Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Peleleja Masesa wakati wa mkutano na vyombo vya Habari.

Bw. Masesa amesema kuwa Matokeo ya Makosa ya watumishi wa Umma waliokata rufaa Tume ya Utumishi wa Umma mwaka 2014/2015 yanaonyesha kuwa kati ya watumishi 135 walikata rufaa walipatikana na makosambalimbali ambapo 54 walipatikana na kosa la utoro kazini.

Bw. Masesa aliongeza kuwa watumishi wengine 16 walishindwa kutekeleza majukumu yao,10 kumdharau mwajiri,8 kughushi nyaraka mbalimbali,8 kufanya malipo kinyume na taratibu,aidha makosa mengine yalikuwa chini ya watumishi 7.

Aidha Masesa aliwataka watumishi wa Umma kujiepusha na vitendo vya rushwa,ulevi,utoro makazini na matendo yote yanayokwenda kinyume na maadili ya utumishi wa umma.“ Utendaji kazi katika utumishi wa Umma huongozwa na sheria,kanuni,taratibu na Miongozo mbalimbali ambayo ipo”Alisisitiza Masesa

Pia Masesa amesema kuwa watumishi watakaoshindwa kuzingatia taratibu zilizowekwa watachukuliwa hatua kali za kisheria na mamlaka za nidhamu katika taasisi husika.

Tume ya Utumishi wa Umma,inawataka waajiri,Mamlaka za ajira na nidhamu na Watumishi wote kuzingatia kanuni za maadili wakati wote wanapotekeleza majukumu yao ili kukuza uchumi,kutoa huduma bora kwa jamii na kulinda amani na utulivu wa nchi.
 Katibu Msaidizi  toka Ofisi ya Rais Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Peleleja  Masesa akiwaeleza waandishi wa Habari(hawapo pichani) leo Jijini Dar es salaam kuhusu mikakati ya Serikali kuhakikisha kuwa watumishi wa Umma wanazingatia maadili ya Utumishi wa Umma ili kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya tano. 
 (Picha na Frank Mvungi-Maelezo).

Katibu Msaidizi  toka Ofisi ya Rais Tume ya Utumishi wa Umma Bi. Celina Maongezi akisisistiza jambo kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es salaam wakati wa mkutano na vyombo vya habari. Kulia ni Katibu msaidizi wa Tume hiyo Bw. Peleleja Masele,kushoto ni Afisa Habari na Mawasiliano wa Tume hiyo Bi Jorlin Kagaruki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...