Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

JESHI la polisi mkoani Pwani linawashikilia watu wawili wanaodaiwa kuhusika na kilimo cha bangi kinyume na sheria huko kandokando ya bonde la mto Ruvu ambalo lipo ndani ya mkoa huo na Morogoro Vijijini eneo la Ngerengere.Aidha jeshi hilo linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine ambao walikimbia na kuacha makazi ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Akizungumzia tukio hilo ,kamanda wa polisi mkoani Pwani,Boniventure Mushongi,alisema watu hao walitiwa nguvuni katika msako,ulioongozwa na mkuu wa polisi wilaya ya Kibaha SSP Mwenda,novemba 14 majira ya asubuhi kwenye bonde hilo na kubaini shamba la bangi lenye hekari tatu.Aliwataja waliokamatwa kuwa ni pamoja na Msahiro Msahiro(45)mkazi wa Usure Shuleni na Hamis selemani (38) mkazi wa Gwata.

Hata hivyo alieleza kuwa shamba hilo lilikuwa likitumiwa na watu hao kwa ajili ya kilimo cha zao hilo haramu la bangi kwa njia ya umwagiliaji ambapo waliliteketeza kwa moto.Kamanda Mushongi alisema ,katika tukio hilo walifanikiwa pia kukamata magunia (mifuko ya sulphate)251 ikiwa na bangi kufuatia kufanyika msako huo .Kamanda huyo alibainisha, wamekamata mbegu za bangi zilizokuwa kwenye magunia 32,mashine za umwagiliaji sita(water pumps)pamoja na mipira yake.

Alifafanua kuwa wamekamata na pikipiki sita zilizokuwa zikitumiwa kusafirisha zao hilo haramu kutoka shambani kwenda kwenye masoko ya biashara hiyo.“Haya ni madawa ya kulevya na sheria za nchi yetu hairuhusiwi kulima,kuuza wala kuyatumia ,sasa leo hii baadhi ya watu wanadiriki kuyalima na kuyasafirisha kupeleka kwenye masoko”

“Bangi linaharibu kwa kiasi kikubwa vijana wetu ambao ni nguvu kazi ya Taifa ,angalia,hekari hizi zote tatu,mbegu za bangi zikiingia mtaani zitaharibu afya na akili za vijana wangapi,”alisema kamanda Mushongi.

Kamanda Mushongi aliomba jamii kupiga vita aina zote za madawa ya kulevya ikiwemo bangi na kuwataka washirikiane na jeshi hilo kuwafichua wale wanaojihusisha na vitendo hivyo.Aliliomba kundi la vijana kuachana na tabia ya kukubali kushawishika ama kujiingiza katika vitendo vya kuvuta bangi na maadili yasiyo mema.

Kamanda Mushongi alisema bado wanaendelea na uchunguzi kwa kushirikiana na kikosi cha kupambana na dawa za kulevya ili kubaini wahusika wakuu na sheria ichukue mkondo wake.
Magunia yaliyopakiwa bangi 251 yakamatwa na Jeshi la polisi mkoani Pwani ambayo yanaonekana yalikuwa tayari kwa kusafirishwa kwenda sokoni.
Pikipiki zipatazo 6 zinazotumika kusafirisha bangi , ambazo zimekamatwa na Jeshi la polisi mkoani Pwani katika msako mkali uliofanyika novemba 14 mwaka huu.
Mashine za kumwagilia na mipira yake sita ambazo zilikuwa zikitumika kumwagilia shamba la bangi lenye hekari 3 huko bonde la mto Ruvu.
(Picha zote na Mwamvua Mwinyi)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...