Judith Mhina - Maelezo
Wazazi Halmashauri ya Kakonko, wafanikiwa kutoa chakula katika shule 59 zilizopo katika Halmashauri hiyo kuamzoa mwaka 2015.
Mkoa wa Kigoma una jumla ya Halmashauri 8 na kati ya hizo ni Kakonko peke yake ndio imefanikiwa kutoa huduma ya uji shuleni. Nikiongea na Waratibu kata kata 5 za
Kakonko Bw Jobson Johnston, Scolastica Andrew, Paschal Mlelema, Eliud
Kayigwe na Samson Sike kwa wakati mmoja wamesema hatukujua kama
Halmashauri nyingine hawana huduma hiyo katika shule zao walidhani ni
mpango wa Mkoa
Hata
hivyo, walisema:” Changamoto walizoziainisha waratibu Kata wa
Halmashauri nyingine hazina mashiko hivyo ni vema wakajithatiti
kuhamasisha wazazi nina hakika wakielewa umuhimu wa chakula shuleni ,
watakubali kuchangia na hatimaye watoto watapata Uji na kutoa huduma
hiyo.
Watoto wa Shule ya Msingi ButaLe Maalum wakipata Chakula cha Mchana shuleni
Waliongeza kwa kusema utafiti wa Shirika la Kimataifa la Watoto UNICEF uliofanyika 2001-2003, ulionyesha
watoto waliowengi wa shule za msingi Mkoa wa Kigoma wamedumaa kwa
kubeba mizigo mikubwa kuliko uwezo wao na kukosa chakula bora, wakati
Mkoa unakila aina ya chakula, na kuongeza mafuta ya mawese matunda
mbogamboga za majani yote yanayopatikana Tanzania yapo Kigoma, , hivyo hakuna sababu ya msingi ya watoto kudumaa.
Mratibu
Kata kiongozi wa Kakonko kwenye Warsha ya Mpango wa Kuinua Kiwango cha
Elimu, Bw Jobson Johnston alisema kila mzazi anachangia kilo 5 ya
mahindi, hivyo shule kupata mahindi zaidi ya mahitaji ya mwaka , ambapo
huuza kiasi kwa ajili ya kupata fedha ya kununulia maziwa, sukari na mafuta ya mawese.
Uji
unaotolewa mashuleni umekuwa na virutubisho bora kabisa kumfanya
mwanafunzi apate usikivu wamasomo darasani, nakuweza kufanya vizuri.Kila
mwanafunzi huja shule na kikombe chake kwa ajili ya huduma ya kupata
uji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...