Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba amewataka vijana wasisite kuleta mabadiliko chanya katika Nchi mana Vijana ndiyo tegemeo la Taifa. 

Ameyasema hayo mjini Unguja alipokua akizindua Baraza la Vijana la Wilaya ya Magharibi A mjini Kisiwani Zanziba.  Amewasishi Vijana watumie baraza hilo kama tanuri ya kutengenezea mbinu za uongozi na pia kama daraja la kuanzishia vikundi vya ujasiriamali na uzalshaji mali na kutengeneza njia mbalimbali za kuinua uchumi na kutowafanya kuwa tegemezi.

Akijibu risala ya Vijana hao ambayo imesomwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo la Vijana Bi Farida Juma ambapo walitaja changamoto zinazowakabili ni pamoja na uhaba wa fedha, Waziri Makamba amelitaka Baraza hilo kufungua akaunti na yeye atawapatia mchango wake wa shilingi milioni mbili.

Awali akimkaribisha Mheshimwa Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Magaharibi A, Mheshimiwa Mwinyiusi Hassan amewataka vijana kuwa nguvu kazi ya Taifa na pia wahakikishe wanalinda na kuheshimu na kuulinda utamaduni wa Nchi yetu.

Wakitoa shukrani zao kwa Mgeni Rasmi Mwakilishi wa Baraza hilo la Vijana walimshukuru Mheshimiwa Waziri kwa kuitikia wito wao wa kumuomba awe mgeni Rasmi katika siku yao hiyo adhimu.
Waziri Wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akihutubia wakati wa uzinduzi wa Baraza la Vijana la Wilaya ya Magharibi ‘A’ mjini kisiwani Zanzibar ambapo alkua Mgeni Rasmi.
Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Baraza la Vijana Wialaya Magharibi A, Waziri Wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akionyesha cheti kama ishara ya uzinduzi wa Baraza la Vijana wilaya ya Magharibi A.
Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Baraza la Vijana Wialaya Magharibi A, Waziri Wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akifurahia jambo pamoja na Mbunge wa Jimbo la Magharibi A, Mh Saada Mkuya, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Bi. Farida Juma na Mkuu wa Wilaya ya Magaharibi ‘A” Mh Mwinyiusi Hassan.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...