WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa, amezindua kituo cha udhibiti na usimamizi wa mifumo ya usambazaji umeme katika jiji la Dar  es salaam kilichoko Mikocheni jijini Dar es Salaam, leo Novemba 16, 2016.
Kituo hicho kipya na cha kisasa, kimejengwa kwa ufadhili wa serikali ya Norway na Tanzania, chini ya mpango wa Mradi wa Uboreshaji Miundombinu ya Umeme jijini.
“Serikali ya awamu ya Tano, iliwaahidi Watanzania, wakati tukiomba kura, ya kwamba, tutaboresha huduma ya umeme kote nchini, na leo hii ni ushahidi tosha tunatekeleza kwa vitendo ahadi zetu.” Alisema Waziri Mkuu ambaye alimwakilisha Rais wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli.
Akimkaribisha waziri Mkuu, Waziri wa Nishati na Madini, Mh. Profesa Sospeter Muhongo amesema, watanzania wanahitaji umeme tena ulio bora, na sasa kituo hicho ni jawabu la kuwapatia umeme ulio bora.

“Kati ya vitu ambavyo sitarajii kuvisikia ni mgao wa umeme, lakini pia bei ya umeme, kuusu bei tutakaa, pembeni na watu wa TANESCO kulizungumzia hili. “ Alitoa hakikisho Waziri Muhongo.Kwa upande wake, Waziri wa Biashara na Maendeleo wa Finland, Mh. Kai Mykkanen, alisema, teknolojia iliyotumika kwenye mitambo ya kituo hicho ni ya kisasa ijulikanayo kama Distribution SCADA System, na inauwezo wa kutambua hitilafu ya umeme kwa haraka na hivyo kurahisisha kurekebisha hitilafu hiyo kwa wakati.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, (katikati) na viongozi wengine kutoka kushoto, Mwenyekiti wa bodi ya TANESCO, Dkt. Alexander Kyaruzi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Juliana Palangyo,Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, (Waziri Mkuu), Waziri wa Biashara na Maendeleo wa Finland, Kai Mykkanen, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Paul Makonda na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba, wakishangilia baada ya kukata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa kituo cha cha udhibiti na usimamizi wa mifumo ya usambazaji umeme katika jiji la Dar  es salaam kilichoko Mikocheni jijini Dar es Salaam, leo Novemba 16, 2016

 Waziri Mkuu na wageni wengine wakitembelea chumba cha mitambo yaudhibiti nausimamizi wa mifumo ya usambazaji umeme Distribution SCADA System
 Waziri Mkuu akitembeela moja ya mitambo inayopatikana kwenye kituo chicho (Server)
 Mtaalam wa mitambo, wa shirika la Umeme Nchini Tanzania, (TANESCO), Bi, Mwajua Turkey, kushoto, akimpatia maelezo waziri mkuu wakati akitembelea kituo hicho muda mfupi kabla ya kukizindua rasmi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...