Na Felix Mwagara, MOHA.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amefanya
mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini, Sara Cooke na kumuakikishia
ushirikiano zaidi kati ya Wizara yake na Ubalozi huo nchini.
Mazungumzo hayo ya zaidi ya saa moja yalifanyika ofisini kwa Waziri Mwigulu,
jijini Dar es Salaam leo ambayo yalijadili masuala mbalimbali ikiwemo
uimarishaji wa ushirikiano kati ya Wizara na ofisi ya Balozi huyo nchini.
Waziri Mwigulu alimuakikishia Balozi huyo kuwa Tanzania itaendelea kuwa
salama kwa kuwa Wizara yake imejipanga vizuri kuendelea kuwalinda raia na mali
zao pamoja na wageni wote waishio nchini.
“Mheshimiwa Balozi nashukuru sana kwa kunitembelea, najisikia furaha kwa ujio
wako na karibu sana wakati wowote, Wizara yangu pamoja na nchi yangu kwa
ujumla tutaendelea kushirikiana nanyi katika masuala mbalimbali,” alisema
Mwigulu.
Hata hivyo, Balozi Sara alimshukuru Waziri Mwigulu kwa mazungumzo
waliyoyafanya na kumuhakikishia ushirikiano zaidi kati ya Uingereza na Tanzania.
Pia kikao hicho kiliudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali
Projest Rwegasira pamoja na Naibu Balozi wa nchi hiyo, Matt Sutherland.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akizungumza na Balozi
wa Uingereza nchini, Sara Cooke (kulia) masuala mbalimbali ya ushirikiano kati
ya Uingereza na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri
Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo.
Balozi wa Uingereza nchini, Sara Cooke (wapili kulia) akimfafanulia jambo
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati), kuhusiana na
masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzania. Mazungumzo
hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto
ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira, na kulia ni
Naibu Balozi wa nchi hiyo, Matt Sutherland.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akimshukuru
Balozi wa Uingereza nchini, Sara Cooke, mara baada ya kumaliza mazungumzo
yao yaliyofanyika ofisini kwa Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo. Balozi
huyo alimtembelea Waziri huyo kwa lengo ya kujadiliana masuala mbalimbali ya
ushirikiano kati ya Tanzania na Uingereza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...