Na Lorietha Laurence-WHSM

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ameeleza kuwa Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 ipo kwa ajili ya manufaa ya kuendeleza sekta ya habari, wanataaluma na Taifa kwa ujumla.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam alipokutana na Balozi wa Denmark nchini  Bw. Einar Jensen ambapo aliuliza kuhusu malalamiko ya waandishi wa habari kupoteza ajira kufuatiwa kuwepo kwa sheria hiyo.

 Mhe. Nape alifafanua kuwa sheria hiyo imetoa kipindi cha muda wa miaka mitano kwa wanahabari wasiokuwa na shahada ya kwanza kuweza kujiendeleza kimasomo ili kukidhi sifa za mwandishi wa habari.

“Sheria hii tayari imeshasainiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambapo kwa  sasa tupo katika utaratibu wa kuweka kanuni mbalimbali ili kufidia sehemu zenye mapungufu” alisema Mhe. Nape

Anaongeza kwa kueleza kuwa kuna faida mbalimbali zinazomsaidia mwandishi kunufaika na sheria hii  ikiwemo bima ya Afya na mfuko wa mafunzo kwa wanahabari ambapo watawezeshwa kupata mkopo wa kujiendeleza kielimu.

Naye Balozi wa Denmark Nchini Bw. Einar Jensen ameipongeza Serikali kwa hatua hiyo nzuri na kuomba ofisi ya Ubalozi wa Denmarm kupatiwa nafasi ya kuweza kukutana na Waziri kwa ajili ya kupata elimu kwa kina kuhusu sheria hiyo.

Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 ilipitishwa na Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  katika mkutano wake wa 5 mjini Dodoma na  kusainiwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  tarehe 16 Novemba mwaka juu.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kushoto) akisalimiana na Balozi wa Denmark Nchini Bw. Einar Jensen (kulia) alipotembelewa na balozi huyo leo Jijini Dar es Salaam ambapo walizungumza kuhusu Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akimueleza jambo  Balozi wa Denmark nchini Bw. Einar Jensen (kushoto) alipotembelewa na balozi huyo leo ofisini kwake  Jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Denmark Nchini Bw. Einar Jensen (kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) wakati wa ziara yake ya kikazi leo Jijini Dar es Salaam.

 Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano kutoka Ubalozi wa Denmark nchini Bibi. Camilla Christensen (kushoto) akizungumza na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) wakati wakijadiliana kuhusu Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Balozi wa Denmark Nchini Bw. Einar Jensen.Picha na Lorietha Laurence

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...