Na Dotto Mwaibale

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi) George Simbachawene amesema ili kusimamia mabadiliko na maendeleo ya nchi na maadili inatakiwa kuwa na kiongozi mbabe na mtemi.

Simbachawene aliyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya uongozi na maadili kwa wahitimu 47 wazalendo waliyoyapata Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere Kivukoni Kigamboni jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza kazi ya ujenzi ya kujitolea ya mwezi mmoja wilayani Mkuranga mkoani Pwani.

Alisema ili kusimamia mabadiliko na maendeleo nchi inatakiwa kuwa na mtu mbabe na mtemi na si kutegemea kundi fulani la watu kwani kwa kufanya hivyo kila kundi litahitaji kupendelewa baada ya kujiona bora kuliko jingine.

Alisema bila kuwa na viongozi wenye maadili nchi haiwezi kusonga mbele kwani tangu kuachwa kwa vijana kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ambako kulikuwa kukitolewa mafunzo ya maadili athari zake zilijitokeza na ndipo kwa kipindi cha miaka 20 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilijikuta kikivamiwa na matajiri wakitaka nafasi mbalimbali za uongozi katika ngazi za ubunge, urais na kuingia katika ujumbe wa mkutano mkuu wa chama kwa njia ya fedha.

“Napenda kusema kuwa tunahitaji mabadiliko makubwa ya kukifumua chama chetu hasa katika mfumo mzima wa kupata viongozi kwani uliopo umetufanya tupoteze baadhi ya nafasi katika majimbo na hata katika uchaguzi ndogo kutokana na mfumo mbaya tulishindwa vibaya baada ya wanachama wetu kumpigia kura mtu mwingine kwa hasira huko vikao vyote vikiendeshwa kwa misingi ya fedha” alisema Simbachawene.
Muhitimu, Ebeneza Emmanuel akipokea cheti kutoka kwa 
mgeni rasmi.
Petro Magoti akikabidhiwa cheti.
Mhitimu Happiness Agathon akipokea cheti.
Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...