Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya UJERUMANI, wamezindua mradi wa huduma za matibabu kwa wanawake wajawazito katika mikoa ya Mtwara na Lindi, unaojulikana kama Mradi wa Tumaini la Mama. 

Akuzungumza katika uzinduzi huo, Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu amewahimiza wanaume kushiriki kikamilufu kwa kuwapeleka wake zao Kliniki na kupata maelekezo kwa pamoja juu ya matunzo ya ujauzito. 

Aidha amewataka wakazi wa mikoa ya Lindi na Mtwara kuzingatia uzazi wa mpango na kuwapunguza watoto wa kike kwenda shule, badala ya kuwaona mapema.Ummy amesema Mradi huo unalenga kuwahuduma wanawake wanatoka katika kaya masikini ambazo zimekuwa zikilazimika kutumia njia zisizo salama za kujufungua kutokana na kukosa fedha za kugharamia huduma hizo katika vituo vya matibabu. 

Kupitia mradi huo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya utawalipia huduma za matibabu wanawake wajawazito wote wa mkoa ya Mtwara na Lindi baada ya kujiandikisha kwenye vituo vya matibabu vilivyosajiliwa karibu nao.Mradi wa Tumaini la mama pia utawapa kadi Mfuko wa Afya ya Jamii CHF wanawake watakaojifungua chini ya mradi huo pamoja na kaya zao. 

Mradi huo ulioanza kutekelezwa ktk mikoa ya Mbeya na Tanga tangu mwaka 2012, umekuwa na mafanikio makubwa ambapo hadi sasa zaidi ya wanawake Laki mbili wamenufaika nao.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu (katikati) kwa kushirikina na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego (kulia) na Mwakilishi Ubalozi wa Ujerumani,Julia Hannig (kushoto) kukata utepe kuzindua rasmi Mradi wa Tumaini la Mama.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akimkabidhi Mayasa Maunda vifaa vya kujifungulia katika uzinduzi wa Tumaini la Mama
Mwimbaji wa muziki wa taarab, Isha Mashauzi akitumbiza kwenye kuzindua rasmi Mradi wa Tumaini la Mama mkoani Mtwara.

Baadhi kina mama waliokabidhiwa vifaa vya kujifungulia wakiwa katika picha ya pamoja katika uzinduzi wa Tumaini la Mama.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...