Na,Jumbe Ismailly,Igunga .

BARAZA la kawaida la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora limeikataa taarifa ya utengenezaji wa madawati ya Halmashauri hiyo,kwa masharti ya kumtaka aliyetoa taarifa ya kumdanganya Rais,Dk.John Pombe Magufuli aende kwenye vyombo vya habari kukanusha taarifa hizo.

Mapema julai,30,mwaka huu wakati wa ziara yake wilayani Igunga,Mkoani Tabora,Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk.John Pombe Magufuli julai,alikabidhiwa taarifa ya wilaya hiyo inayosema wilaya ya Igunga haina upungufu wa madawati na kibaya zaidi kwa mujibu wa taarifa hiyo ilikuwa na ziada ya madawati mia mbili.

Maamuzi ya Madiwani hao yanafuatia taarifa ya utengenezaji wa madawati iliyotolewa na afisa elimu wa wilaya hiyo, Mwisungi Kigosi kwenye mkutano wa kawaida wa baraza hilo kuonyesha mabadiliko ya takwimu zilizotolewa kwa Rais na walizosomewa madiwani hao.

Wakichangia kwa nyakati tofauti hoja hiyo baadhi ya madiwani,diwani wa viti maalumu CHADEMA,Anna Nyarobi,Charles Bomani wa kata ya Igunga,Gedi Nkuba wa kata ya Nguvumoja na Henry Saidi wa kata ya Mwamala walisema kuwa kuokana na taarifa hiyo kukinzana,kuwa na mkanganyiko na taarifa iliyotolewa kwa Rais na kutokuwa vizuri,hawatakuwa tayari kuipokea taarifa hiyo na kuirudisha kwenye kamati ya madawati wakaipitie tena upya na kisha kuipeleka kwenye baraza maalumu la madiwani.

Anna Nyarobi ni diwani wa viti maalumu kupitia CHADEMA akichangia hoja hiyo alipendekeza kwamba watu waliotoa taarifa za uongo waende kwenye vyombo vya habari na kukanusha taarifa hiyo kwa kusema kuwa taarifa waliyotoa ilikuwa ni ya uongo,ili waweze kurudisha imani za wananchi kwa madiwani wao.

Hata hivyo diwani,Gedi Nkuba alibainisha kuwa kutokana na kuwepo kwa upungufu wa madawati,alishauri Mkaguzi wa ndani afuatilie taarifa ya madawati hayo pamoja na tathimini ya fedha zote zilizokusanywa kwa ajili ya utengenezaji wa madawati hayo iweze kubainika.

Naye diwani wa kata ya Mwamala,aliyekuwa mmoja wa wajumbe wa Tume ya kufuatilia utengenezaji wa madawati,Henry Saidi kwa upande wake alibainisha kwamba,baada ya kubaini kuwepo kwa mianya ya ufujaji wa fedha za madawati ya Halmashauri ya Igunga,walishindwa kuendelea na mchakato huo wa utengenezaji wa madawati.
Ni Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora,Bwana Revocatus Kuul(wa kwanza kutoka kulia) akiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,Bwana Peter Onesmo wakati wa mkutanao wa kawaida wa baraza la madiwani walipokuwa wakisomewa taarifa ya utengenezaji wa madawati,taarifa ambayo waliikataa baada ya kubaini kuwa taarifa iliyotolewa julai,30,mwaka huu kwa Rais,wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk.John Pombe Magufuli ilikuwa ya uongo.
Mkuu wa wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora,Bwana John Mwaipopo akifungua mkutano wa kawaida wa barazaa la madiwani wa Halmashauri yaa wilaya ya Igunga.
baaddhi ya madawati yaliyotengenezwa na Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora kwa ajili ya kusambaza katika shule za msingi na sekondari zilizopo kaatika wilaya hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...