Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii .

KUFUATIA Agizo la Rais John Pombe Magufuli la kutaka  Wafanyabiashara ndogondogo ‘machinga’ wasibugudhiwe na watafutiwe maeneo rasmi ya kufanyia biashara ambayo yatakuwa na mazingira rafiki, Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema amesema  maeneo ya wafanyabiashara hayo tayari yameshatengwa huku yakiwa na mazingira ya kuweza kufanya biashara.

Mjema ameyasema hayo leo wakati wa ziara ya  kuzungukia masoko ambayo wanatarajia  kuwahamishia wafanyabiashara walio katika Manispaa ya Ilala, ikiwemo soko la Kivule na Kerezange ambapo kwa sasa yapo tayari huku akiahidi kushughulikiwa kwa changamoto ya miundombinu ya barabara na stendi ya mabasi.

Mjema amesema katika kuwa na mazingira mazuri ya kufanyia biashara ni pamoja kuwa  kituo cha Daladala ambapo abiria wanashuka na kupata mahitaji yao katika masoko.Amesema  soko la Tabata Muslim liko katika hatua za mwisho mpaka mwezi wa 12 masoko yote yatakuwa katika mazingira rafiki ya kufanya wafanyabiashara ndogodogo  waweze kufanya biashara zao. 

Mjema amesema kutokana na kuondoka kwa wafanyabiashara hao kutakuwepo wa eneo moja la  barabara ambazo wafanyabiashara wataruhusiwa kufanya biashara kando kando ya barabara  kwa siku za Ijumaa, Jumamosi  pamoja na  Jumapili kuanzia majira saa sita mchana kwa wafanyabiashara .

Mitaa ya Lumumba na Mkunguni itatumika kufanya biashara kwa siku za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili eneo hilo linauwezo wa kukaa  zaidi ya wafanyabiashara 1800.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amesimamia uadikishwaji wa machinga waliokuwa wafanyabiashara  kandokando ya barabara za mabasi yaendayo kasi na kuwataka ambao hawajajiandikisha wajiandikishe  mapema ili wapatiwe maeneo rasmi.
 Wafanyabiashara ndogondogo wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Ilala,Sophia Mjema leo jijini Dar es Salaam.
 Wafanyabiashara Ndogondogo wakijiandikisha majini yao ili wapatiwe maeneo rasmi ya kufanyia biashara ambayo yatakuwa  na mazingira rafiki, leo jijini Dar es Salam.
 Mkuu wa wilaya ya Ilala,Sophia Mjema akizungumza na waandishi wa habari, leo Jijini Dar es Salaam katika soko la kuu la Kelezange lililopo kata ya Kivule, ikiwa ni ziara yake ya kutembelea masoko ambayo wafanyabiashara ndogondogo watapelekwa kufanya biashara leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Sophia Mjema akizungumza na viongozi wa wafanyabiashara ndogondogo ‘Machinga’  katika soko la kuu la Kelezange lililopo kata ya Kivule leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...