Mbunge wa Jimbo la Namtumbo ambae pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amewahakikishia wananchi wa Kata ya Mchomoro Wilayani humo kuwa jengo la Zahanati ya kijiji hicho litakamilika na kuanza kutoa huduma mwezi Machi mwakani kama ilivyopangwa. 

Jengo hilo ambalo ujenzi wake unatokana na kuharibika kwa jengo la zamani kulikosababishwa na ujenzi wa barabara ya Songea- Tunduru linatarajiwa kuendelezwa ili kuwa kituo cha afya na hivyo kuhudumia idadi kubwa ya wananchi wa Kata hiyo. 

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo hilo Eng. Ngonyani amewakabidhi wasimamizi wa ujenzi huo fedha kwa ajili ya kukamilisha hatua upauaji wa jengo hilo na kusisitiza umuhimu wa matumizi sahihi ya fedha hizo ili ziwiane na ubora wa kazi. 

“Hakikisheni mnazingatia makubaliano ili zoezi la kuezeka jengo hili la Zahanati likamilike kabla ya Januari na hivyo kuwezesha zahanati hii kuanza kazi mapema mwezi Machi”. Amesema Eng.Ngonyani. 
Muonekano wa jengo la zahanati ya Mchomoro wilayani Namtumbo ambayo ipo katika hatua za za mwisho za ujenzi wake, Zahanati hiyo inatarajiwa kuendelezwa ili kuwa kituo cha afya ya kata hiyo.
Mbunge wa Namtumbo Eng. Edwin Ngonyani akitoa maelekezo kwa mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa zahanati ya Mchomoro mara baada ya kukagua ujenzi wa zahanati hiyo
Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa zahanati ya Mchomoro wakijadiliana jambo mara baada ya kupokea fedha kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Eng. Edwin Ngonyani kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa zahanati hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...