Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi katika mradi mkubwa wa maji kwenye mji Nansio katika kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza mradi ambao utahudumia wananchi elfu 61.

Makamu wa Rais ambaye amesafiri kwa takribani masaa Matatu na meli ya MV Nyehunge II katika Ziwa Victoria kwenda kisiwa Ukerewe kwa mara ya kwanza tangu ashike wadhifa huo,amewahimiza wananchi hao wautunze mradi huo ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa tatizo na uhaba wa maji safi na salama katika kisiwa hicho.
Mradi huo ambao unaojumuisha kazi za uboreshaji wa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira unatekelezwa chini ya umefadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na serikali ya Tanzania katika miji ya Sengerema,Geita na Nansio – Ukerewe kwa gharama ya Dola za Kimarekani milioni 30.4 ambapo serikali ya Tanzania imechangia mradi huo Dola za Kimarekani milioni nne.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewaahidi wananchi kuwa serikali ya awamu ya Tano unamikakati mizuri inayolenga kuondoa tatizo la maji kote nchini  ili kusaidia wananchi hao hasa wanawake kutumia muda mwingi kufanya kazi za maendeleo kuliko kutafuta maji. 
Akihutubia mamia ya wananchi  wa kisiwa cha ukerewe kwenye kijiji cha Kagunguli mkoani Mwanza mara baada ya kuweka mawe ya msingi katika miradi miwili ya ukiwemo mradi wa maji na ujenzi wa chumba cha upasuaji katika kituo cha afya cha Kagunguli, Makamu wa Rais amewapa pole wananchi wa kisiwa hicho baada ya kukumbwa na tufani ya kimbunga cha upepo iliyotokea tarehe 04 Novemba 2016 na kusababisha uharibifu mkubwa ikiwemo nyumba za watu kubomoka.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili Nansio wilayani Ukerewe kwa meli ya MV. Nyehunge II ambapo alikuwa na kazi za kuweka jiwe la msinggi kwenye mradi wa maji wa Nebuye pamoja na kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Chumba cha Upasuaji kituo cha Afya Kagunguli na kuhutubia wananchi
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akiambatana na viongozi mbali mbali katika kukagua  mradi mkubwa wa maji wa Nebuye wilayani Ukerewe mkoa wa Mwaza
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akisoma maandishi yalioandikwa kwenye jiwe la msingi la mradi mkubwa wa maji wa Nebuye wilayani Ukerewe mkoa wa Mwaza.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akiwapungia wakazi wa kijiji cha Kagunguli wakati akiwasili tayari kuhutubia wakazi wa kijiji hicho.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa kijiji cha Kagunguli wilayani Ukerewe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...