Judith Mhina - MAELEZO.
Nidhamu katika Utumishi wa Umma inayosisistizwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Imeiweka Tanzania
katika ramani ya dunia.
Hayo yamesemwa na Balozi Christopher Liundi katika mahojiano
kwa njia ya simu yaliyofanyika jana jumapili. Mheshimiwa Balozi Liundi alisema;
Tanzania sasa dunia nzima, na ndivyo ilivyokuwa kwa Tanzania
utakumbuka enzi za Baba wa Taifa. Rais wetu anaifufua ile ari na kurejesha heshima iliyokuwepo hapo awali ;Ameeleza kwamba nidhamu katika kila kitu ni jambo la msingi
sana, iwe katika utumishi wa Umma au wa Sekta binafsi, barabarani, Nidhamu
inatakiwa itoke moyoni mwako na ufurahie hali ya kuwa na nidhamu. Nidhamu
katika Utumishi wa Umma ni lazima ni msingi kwa vijana wetu katika kupata ajira
bila ya malamiko kutokana na Waajiri na wadau wengine kuwa vijana hawafanyi
kazi au wavivu, hawana nidhamu, na viwango.
Balozi Liundi amefafanua kuwa, enzi za Baba wa Taifa
unapokwenda popote duniani, ukisema niketoka Tanzania kila mtu anajua Mtanzania
ni mkweli, muwazi na ana nidhamu ya hali
ya juu. Mtanzania hawezi kupokea wala kutoa rushwa, hashiriki kwenye masuala
yoyote ya kuiharibia heshima nchi yake, mwenye kutumia madaraka yake vizuri, na
asiyefuja mali ya umma.Amesema wakati umefika kwa Watanzania kumuunga mkono Rais
wetu katika kuhakikisha kwamba nidhamu katika utumishi wa Umma inakuwepo.
Akiongea kuhusu miaka 55 ya Uhuru wa Tanganyika Balozi Liundi
amesema kauli ya Rais Magufuli la kutaka Taifa liondokane na umasikinini kwa
kufufua au kujenga viwanda vidogo vya kati na vikubwani lazima utekelezwe.
Balozi Liundi amempongeza Rais kwa jitihada zake za kuwaweka
katika utayari wafanyabiashara binafsi wa Tanzania katika kujenga viwanda.
Akiongea na wananchi alipokwenda kufungua kiwanda cha matunda cha Azam cha
Salim Said Bahkresa atahakikisha changamoto zilizopo kama umeme kwa kuagiza
TANESCO wamfungie umeme na kumpa shamba la hekari 1000 bure ili kupanda miwa
kwa ajili ya kuzalisha sukari. “Kazi ya Serikali ni kuweka mazingira mazuri ya
uwekezaji ambao kwa vitendo Rais amelithibitisha hili”.
Pia
nampongeza kwa kuanzisha mfumo unaomtaka kila mfanyabiashara kuwa na mashine za
kulipa kodi: “Mpaka sasa imefikia mahali nchi nyingine za nje wameanza kuiga
utendaji wa kazi wa Rais wetu hili ni jambo la kujivunia”. Hivyo tumuunge mkono
katika hii vita ya ukusanyaji kodi.
Tunapoadhimisha miaka 55 ya Uhuru wetu tukumbuke kauli ya
Mwalimu Nyerere alisema: “ UHURU NA KAZI”,
ni kweli kabisa lazima tufanye kazi kama anavyosisitiza Rais wetu Magufuli “HAPA KAZI TU”. Maendeleo hayaji kwa
kupiga hadithi ni lazima watu wafanye kazi na asiyefanya kazi na asile.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...