Na Jacquiline Mrisho 
– MAELEZO.
Mbali na jitihada za makusudi za Serikali na wadau wa mapambano dhidi ya UKIMWI nchini bado hali siyo ya kuridhisha ambapo Jiji la Dar es Salaam linashika nafasi ya Sita barani Afrika kwa maambukizi ya ugonjwa huo.
Dar es Salaam ambalo ni Jiji kubwa kuliko yote Tanzania linakadiriwa kuwa na watu 210,000 wanaoishi na virusi vya UKIMWI ambapo kati yao asilimia 58 ni wanawake, na kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 idadi ya wakazi wa jiji hilo inakadiriwa kuwa Milioni 5.
 Kwa mujibu wa taarifa ya hali ya UKIMWI duniani kutoka Shirika la Mpango wa UKIMWI la Umoja wa Mataifa - Tanzania (UNAIDS) kwa mwaka 2015, Jiji la Dar es Salaam limekuwa kati ya majiji Barani Afrika yenye kiwango kikubwa cha maambukizi ya UKIMWI.
Afisa wa UNAIDS Tanzania, Fredrick Macha (pichani) anasema asilimia 16 ya maambukizi yote mapya Tanzania Bara yanatokea katika jiji la Dar es Salaam ambapo kwa wanawake wenye umri mdogo wa miaka 15-24 kiwango cha maambukizi kimefikia asilimia 7%,sababu kubwa ikiwa ni kujiingiza katika ngono wakiwa na umri mdogo pamoja na biashara ya ukahaba.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA                                                                                      

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...