Na Rhoda Ezekiel -Globu ya Jamii,Kigoma.

JESHI la polisi Mkoani Kigoma limefanikiwa kukamata risasi 408 za bunduki zilizo kuwa zikimilikiwa na Mtu mmoja ambaye jina lake halikutajwa mkazi wa Kijiji cha Makere Wilayani kasulu Mkoani Kigoma.

Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake leo Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Kigoma,DCP Fredinand Mtui alisema mnamo tarehe 5Desemba majira ya 08:20 huko maeneo ya makere Center katika kijiji cha Makere askari wakiwa doria walipokea taarifa kutoka kwa raia wema wanao chukia uhalifu kuwa kuna mtu wana wasiwasi nae kuwa anamzigo usio kuwa wa kawaida.

Mtui alisema Askari walianza ufuataliaji na kufanikiwa kukamata mtuhumiwa mmoja ambaye jina lake limehifashiwa kwa shughuli za kiusalama, alipo fanyiwa upekuzi mtuhumiwa huyokatika Sanduku lake alilokuwa amebeba alikutwa akiwa na risasi 408 za bunduki aina ya SMG/SAR alizokuwa amezifunga ndani ya nguo zake .

Aidha Mtui alisema upelelezi bado unaendelea ,Mtuhumiwa atapelekwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria pindi upelelezi utakapo kamilika ilikutoa fundiaho kwa wananchi wengine wanao nunua siraha kwa lengo la kufanyia uhalifu.

"nichukue fursa hii kuwaasa wahalifu wanao jihusisha na biashara ya kuuza na kununua risasi na siraha nyingine waache biashara hiyo, wafanye kazi nyingine ambazo zinatambulika kisheria vyombo vya ulinzi na usalama viko imara kuwatafuta wahalifu hao na kuwachukulia hatua za kisheria,"alisema Mtui.

Sambamba na tukio hilo alisema mnamo tarehe 6Desemba huko maeneo ya Mwanga Vamia Manispaa ya Kigoma ujiji Hussen Athuman (36) Mkazi wa mwanga Vamia alikutwa chumbani kwake akiwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya katani. 

Mtui alisema usiku wa tarehe5 marehemu alimpigia simu Dada yake na kudai kuwa walikuwa na ugomvi na mkewe ugomvi huo uliopelekea mkewe kuondoka siku nne zilizo pita , na kumwambia amueleze kaka yake kwamba atachukua maamuzi magumu.

Alisema chanzo cha kujinyonga ni ugomvi baina ya baina ya marehemu na mkewe, mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospital ya rufaa maweni kusubili kukabidhiwa kwa ndugu kwa taratibu za mazishi.
 Risasi 408 za bunduki zilizo kuwa zikimilikiwa na Mtu mmoja ambaye jina lake halikutajwa, mkazi wa Kijiji cha Makere Wilayani kasulu Mkoani Kigoma. 
Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Kigoma,DCP Fredinand Mtui akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani),kuhusiana na tukio hilo la kukamatwa risasi za moto 408,zilizokuwa zikimilikiwa na mtu mmoja mkoani humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...