Na Amina Kibwana,Globu ya Jamii
Kampuni ya Uwekezaji ya Taifa (NICOL) inatarajia kurudi upya
mara baada ya kuingia hasara ya sh. Billion 10 pamoja na kukabiliana na kesi Mbalimbali
ikiwemo kupinga maamuzi ya wanahisa kuchagua
uongozi pamoja na maamuzi ya kusitishwa kwa mkutano mkuu uliolenga kuzungumzia maswala
ya mahesabu na muelekeo wa Kampuni.
Akizungumza na waandishi wa Habari Mwenyekiti wa
NICOL Dk. Gideon Kaunda amesema kuwa kesi ya mwisho ya 41 iliamuliwa
mahakamani mara baada ya Mlalamika makamu
mwenyekiti wa TPSF Salum Shamte kutokuhudhuria mahakamani na hoja hizo
zilikataliwa na Mahakama kuamua kuwa mkutano huo ulikuwa wa halali na
ambapo
mnamo Novemba 26 mkutano huo uliendelea.
“Mkutano ulikwenda vizuri ambapo zaidi ya watu 300 kutoka
mikoa mbalimbali walihudhuria pamoja na mashirika mbalimbali ya umma ambayo
yalikuwa yamewekeza wakiwemo PSPF,
walifanikiwa kuhudhuria”. Alisema Kaunda
Aidha alisema kuwa Kampuni hiyo iliingia hasara kutokana na uongozi uliopita kuwa na malimbikizo ya sh.
Billion 10 kutokana na mahesabu yaliyofanywa, ambayo taarifa ilionesha
kuwa kampuni ilikuwa inapata faida kwa wakati huo sio sahihi,pamoja na
kutokufuatwa kwa sheria na utovu wa nidhamu.
Kwa upande wake Mtendaji
Mkuu wa NICOL Adam Wanuza
amesema kuwa kuwa pamoja na hasara hiyo,ukiwemo uwekezaji mbovu umechangia kutokana
na makampuni mbalimbali kuchukua mkopo katika Kampuni ya Nicol.
Naye
Naibu Waziri Mstaafu katika sekta ya Uchukuzi ambaye pia ni Mtaalamu
katika Masuala ya Biashara Dk. Athumani Mfutakamba amesema kuwa
kufanikiwa kwa Mkutano huu ni ishara tosha ya kuzaliwa upya kwa NICOL
katika jitihada za Kampuni ya uwekezaji ya kizalendo na jitihada hizi
lazima ziungwe mkono na wazalendo wote wanaotaka maendeleo ya uchumi wa
Taifa la Tanzania katika fursa mbalimbali.
Kampuni
ya Nicol itarudi Rasmi kupitia uongozi mpya sambamba na kuanza kutoa
elimu Maalumu kwa wawekezaji katika soko la Hisa mnamo mwanzoni mwa
mwaka 2017.
Mwenyekiti wa kampuni ya Uwekezaji wa Taifa (NICOl) Bw. Gideon Kaunda kulia akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es salaam mara baada ya kupata uongozi mpya wa kampuni hiyo ulioteuliwa rasmi hivi karibuni na bodi ya NICOL kushoto ni Mtendaji Mkuu Bw. Adam Wamunza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...