Na Anthony John- Glob ya Jamii.

TAKWIMU zinaonyesha kuwa maambukizi mapya ya ukimwi yamepungua ikiwemo kwa watoto kwa asilimia 50% japokuwa bado ni janga kubwa kwa Dunia,Afrika na Tanzania hivyo nguvu zaidi inahitajika kupambana na ugonjwa huo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo hii Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania Leonard Maboko amesema kuwa mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi yanatakiwa kuwa endelevu haswa katika maeneo yanayoonyesha kuathirika zaidi ili kutokomeza maambukizi mapya.

" wakati maambukizo mapya yameshuka kwa asilimia 50 miongoni mwa watoto duniani 290,000 wapya waliambukizwa mwaka 2010 na watoto wapya 150,000 waliambukizwa Mwaka 2015 maambukizo mapya kwa watu wazima hayajashuka tangu 2010 duniani" amesema Maboko.

Aidha maboko ameongeza kuwa Dunia imejiweke lengo la kutokomeza Ukimwi kama janga ifikapo mwaka 2030 kupitia Shirika la umoja wa mataifa linalo ratibu mapambano dhidi ya Ukimwi (UNAIDS) kwakuanza kutoa dawa za kufubaza virusi vya ukimwi mara tu mgonjwa anapogundulika kuwa na Ugonjwa huo.

Wakati Huo Huo Mkurugenzi huyo alitumia fursa hiyo kuwaasa watanzania kutokubweteka na mafanikio ya takwimu kushuka kwa maambukizi ya virusi vya Ukimwi na badala yake kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Dkt Leonard Maboko (Katikati)akiwa na Mkuu wa kitengo cha Sheria Bi Elizabeth Kaganda(Kushoto)Pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Uraghibishi Bw Jumanne Issango(Kulia)Wakiongea na Waandishi wa Habari Kuhusu Takwimu za Hali ya Virusi vya  Ukimwi na Ukimwi kwa Tanzania kwa Kulinganisha na hali ya Dunia na ya Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika.
 Akizngumza na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Mikutano wa TACAIDS leo jijini Dar es salaam.Picha na Yasir Adam Blog ya Jamii⁠⁠⁠⁠

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...