Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi, Prof. Idrissa Mshoro akiwasili katika viwanja vya chuo hicho kwa ajili ya kuhudhuria katika mahafali ya 10 ya chuo hicho yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
 
 Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi, Mhe. Cleopa Msuya akimtunuku mmoja wa wanafunzi wa shahada ya Udaktari wa Falsafa (PhD) aliyoipata katika chuo hicho. Mahafali hayo yamefanyika jana Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya chuo hicho.
 Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi, Mhe. Cleopa Msuya (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine waliohudhuria kwenye mahafali ya 10 ya chuo hicho akiwemo Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho, Prof, Evelyne Ambede (wa pili kushoto), wa tatu kulia ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya. Mahafali hayo yamefanyika jana Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya chuo hicho.
 
 Baadhi ya wahitimu shahada ya Udaktari wa Falsafa (PhD)   katika chuo hicho wakiwa katika viwanja vya chuo. Mahafali hayo yamefanyika jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wa shahada na stashahada waliohitimu katika chuo hicho wakiwa katika viwanja vya chuo. Mahafali hayo yamefanyika jana jijini Dar es Salaam. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...