Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip
Mpango (Mb) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Jengo la pili la Taaluma lenye
ghorofa 7 la Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Kampasi Kuu ya Dodoma,
lililogharimu shilingi Bilioni 10.3.
Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo hicho Prof. Razack
Lokina na kushoto kwake ni Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Dkt.
Frank Hawassi wakifurahi kwa pamoja mara baada ya uzinduzi huo.
Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akiangalia viatu vya ngozi vilivyotengenezwa
na mjasiliamali mdogo Bw. Stephano Chifwaguzi (nayeonesha bidhaa ya ngozi
kiunoni) baada ya kuwezeshwa kiutaalamu na Chuo cha Mipango na Maendeleo
Vijijini, kwa ufadhili wa Jumuiya ya Ulaya, wakati wa mahafali ya 30 ya Chuo
hicho Kampasi Kuu ya Dodoma.
Meza Kuu
ikiongozwa na Mgeni Rasmi, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango
(Mb) akifurahia mahafali ya 30 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini,
yaliyofanyika Kampasi Kuu ya Dodoma katika eneo la Miyuji-mkoani humo.
Wajumbe wa Baraza la kumi na la tisa la uongozi
wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo
Vijijini wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa Mahafali ya 30 ya Chuo cha Mipango
na Maendeleo Vijijini Kampasi ya Dodoma, iliyoko katika eneo la Miyuji, mkoani
humo.
Wahitimu wa Chuo
cha Mipango ya Maendeleo Vijijini pamoja na wageni waalikwa, wakiimba wimbo wa
Taifa wakati wa Mahafali ya 30 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika eneo la
Miyuji, mkoani Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...