Na Woinde Shizza,Arusha

Mahakama ya hakimu mkazi mkoani Arusha imefuta kesi iliyokuwa ikimkabili aliyewahi kuwa mwenyekiti wa UVCCM mkoani hapa, Lengai Ole Sabaya baada ya upande wa Jamhuri kusema kuwa haitaki kuendelea na kesi hiyo

Akitoa maelezo ya kesi hiyo Hakimu wa Mahakama ya Hakimu mkazi ya mkoa wa Arusha, Gwantwa Mwangoka amesema kuwa shauri hilo lililetwa na serikali mahakamani hapo, hivyo mahakama imeona haja ya kuendelea na shauri hilo.

Awali wakili upande wa Jamhuri, Grace Makidenya aliwasilisha ombi mahakamani hapo la kuiomba mahakama kuiondoa kesi hiyo
 
aliyewai kuwa Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha Lengai Ole Sabaya (katikati) akiwa anatoka mahakamani (picha na maktaba).
 
Kwa upande wake wakili anayemtetea Sabaya amesema kuwa ipo mamlaka anayokuwa nayo DPP kuondoa shauri mahakamani hivyo kesi iliyokuwa inamkabili imefutwa hivyo hakuna kesi inayomkabili tena.

Wakati huohuo
mtuhumiwa huyo alikamatwa kwa mujibu wa sheria namba 255 ya  mwenendo wa makosa ya jinai nchini. 

Mara baada ya kufutiwa kesi na mahakama hiyo, Lengai Ole Sabaya alikamatwa tena na polisi ,mwandishi wa habari hizi alifanya jitihada za kumtafuta kamanda wa polisi mkoani hapa Charles Mkumbo  ili aweze kuzungumzia sakata la kukamatwa kwa Sabaya, Kamanda amesema kuwa hiyo ni teknikali ya kisheria bali kesi ni hiyohiyo na jeshi la polisi linafanya taratibu zao na zikikamilika watamrudisha tena mahakamani.

Miezi kadhaa iliyopita aliyekuwa mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi ‘UVCCM’ Arusha, Lengai Ole Sabaya alishtakiwa kwa kosa la kujifanya ofisa usalama wa Taifa na kughushi kitambulisho cha usalama wa taifa. 

Kesi hiyo imetolewa maaamuzi na mahakama ya hakimu mkazi Arusha leo December 14 2016 ambapo imemuachia huru Lengai Ole Sabaya baada ya upande wa Jamhuri kusema hawana nia ya kuendelea na kesi hiyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...