WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameugiza uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya  Ngorongoro (NCAA), kumpelekea nyaraka zote zilizotumika katika kumhamisha faru maarufu kwa jina la John katika hifadhi hiyo ifikapo Desemba 8, 2016.

Ametoa agizo hilo leo (Jumanne, Desemba 6, 2016) alipotembelea Ofisi za makao makuu ya NCAA, zilizoko wilayani Ngorongoro mkoa Arusha  wakati akizungumza na watumishi wa mamlaka hiyo pamoja na Wajumbe wa  Baraza la Wafugaji ikiwa ni  sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani hapa.
"Nina taarifa zenu kuwa mlimhamisha kwa siri faru  John kreta na kumpeleka  V I P Grumet  Serengeti Desemba 17, 2015 na mliahidiwa kupewa sh. milioni 200 ambapo  mkapewa sh.  milioni 100 kwa ahadi ya kumaliziwa sh. milioni 100 nyingine baadaye,".

 “Naomba niletewe nyaraka zote zilizotumika kumuomba na kumuondoa faru huyo na barua zilizotumika kujadili suala la faru John. Nasikia amekufa...Naomba pembe ziletwe ofisini na iwapo itathibitika aliondoka bila ya kufuata taratibu wahusika wote watachukuliwa hatua kali za kisheria,”.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amepiga marufuku tabia ya baadhi ya watumishi wa mamlaka hiyo ambao wanawakabidhi watoto kupeleka ng’ombe wao ndani ya kreta. “ Watumishi wa Ngorongoro ndiyo wanaopeleka ng’ombe ndani ya kreta na si wenyeji. Sasa ni marufuku na tutakayemkuta hatutakuwa na msamaha naye,”.

Amewataka watumishi hao kuhakikisha wanakuwa waadilifu na wanafanyakazi kwa kufuata misingi ya kiutumishi na kuacha tabia za kuendekeza rushwa na wizi.Wakati huo huo Waziri Mkuu amemsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa NCAA, Sezzary Simfukwe kutokana na tuhuma za ubadhilifu wa fedha zinazomkabili na tayari  anahojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

"Haiwezekani mtumishi  awe anachunguzwa  na TAKUKURU halafu aendelee kuwa ofisini si atavuruga uchunguzi? Asimamishwe kazi kuanzia leo mpaka hapo uchunguzi utakapokamilika na aikibainika kwamba hana hatia atarudi kazini,” alisema.Pia Waziri Mkuu alimtaka Mkurugenzi Mkuu wa NCAA, Fred Manongi kueleza zilipo sh. bilioni moja zilizotolewa na Rais wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Kikwete  kwa ajili ya kujengea ranchi  ya wafugaji wa tarafa ya Ngorongoro.

Akijibu swali hilo Manongi alisema wakati Rais Kikwete anatoa fedha hizo alikuwa bado hajateuliwa kushika wadhifa huo, ambapo Waziri Mkuu alimuagiza Mkurugenzi huyo  kufanya uchunguzi juu ya fedha hizo na kisha kumpelekea taarifa.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMANNE, DESEMBA 6, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwenye ukumbi wa Ofisi za Mamlaka hiyo Desemba 6, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwenye ukumbi wa Ofisi za Mamlaka hiyo Desemba 6, 2016.
Baadhi ya watumishi wa Mamlka ya Hifadhi ya Ngorongoro wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Ofisi za Mamlaka hiyo Desemba 6, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...