Na Woinde Shizza,Meru

KAMANDA wa Polisi mkoa wa Arusha, Naibu Kamisha wa Polisi (DCP) Charles Mkumbo amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa Wilson Elius anayeshikiliwa kwa kosa la ubakaji lililotokea Novemba 13 eneo la USA River Mkoani Arusha.

Kamanda Mkumbo alimesema kuwa mtuhumiwa alikamatwa kwa rb namba RB/R/4250/2016 na atafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika.

Mwanafunzi huyo wa  kidato cha tatu katika shule ya sekondari (imehifadhiwa jina)mkoani Arusha ameshindwa kuendelea na masomo baada ya kubakwa na kutelekezwa kwenye korongo la mchanga .

Akielezea tukio hilo mwanafunzi huyo ambae amehifadhiwa jina kwa sababu za kimaadili alisema kuwa tukio hilo lilitomkea Novemba 13 majira ya saa 12.30 alipotoka kwa kinyozi.

Alisema kuwa ghafla akiwa anarudi nyumbani alikutana na mtu huyo aliyemfanyia kitendo hicho na kuanza kumkaba shingoni na kumziba mkono ili asitoe sauti na ndipo alipomfanyia kitendo hicho cha ukatili ambacho kimemfanya ashindwe kuendelea na masomo yake vizuri.

"Nilijitahidi sana kupiga kelele ila kutokana na alivyokuwa amenikaba shingoni alinifanyia kitendo hiki kikatili ambacho kimenipelekea nishindwe kuendelea na masomo yangu kwani baada ya vipimo nimeonekana aliniumiza sehemu nyingi ikiwemo hata kifua changu"alisema mwanafunzi huyo.

Kwa upande wa mama mzazi wa mwanafunzi huyo aliyejitambulisha kwa jina la Rambikiaeli Akyoo alisema kuwa kutokana na vitendo vya ukatili kukithiri kwa mabinti zao ni vyema serikali ikawa inawachukulia hatua mapema wanaohusika kwani tangu akamatwe mtuhumiwa huyo na kupelekwa kituoni bado hajasomewa shtaka linalomkabili hivyo kufanya wanaohusika na vitendo hivyo kuona wako sawa kwa vile hakuna hatua kali inayochukuliwa mapema dhidi ya matukio hayo

Nae Mkuu wa shule hiyo, Nkoe Nicolaus alisema kuwa tukio hilo limemfanya mwanafunzi huyo aathirike kisaikolojia kwani tangu afanyiwe ukatili huo ameshindwa kuendelea na masomo yake vizuri hivyo anawashauri wazazi wa binti huyo kumuhamisha shule hiyo na kumuhamishia nyingine ili kimbadilisha mawazo ya kifikra.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji cha kitefu tanesc,o Samweli Matayo alikiri kutokea kwa tukio hilo katika kitongoji chake na kusema kuwa mara baada ya taarifa walifanikiwa kumtia hatiani mtuhumiwa aliyetambulika kwa jina la Wilson Elias ambae ndie aliyehusika na ukatili huo na kumfikisha katika kituo kidogo cha Polisi Usa River ili kukabiliana na shutuma hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...