Habari  Picha na Woinde Shizza,Arusha.

Aliyekuwa mkuu wa majeshi na Mwenyekiti wa bodi ya TANAPA,Jenerali Mstaafu Geogre Waitara anatarajiwa kuongoza  msafara wa zoezi la kupanda mlima kilimanjaro desemba 5 hadi 10 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 55 ya  uhuru wa tanzania.

Aidha katika msafara huo wa kupanda mlima kilimanjaro watakuwepo pia wanajeshi kutoka Jeshi la wananchi Tanzania pamoja na wanahabari ambao watakuwa wanahabarisha jamii kuhusiana na tukio hilo.

Akizungumza na vyombo vya habari Mkurugenzi mkuu wa TANAPA ,Allan Kijazi alisema kuwa mwaka huu Tanzania itaadhimisha miaka 55 ya uhuru na hivyo shirika hilo ikishirikiana na kampuni ya utalii ya Zara pamoja na bodi ya utalii (TTB) kuandaa zoezi la kupanda mlima kilimnajro ili kuhamasisha  Watanzania kuvifahamu vivutio vya utalii.

Alisema kuwa zoezi hilo la upandaji mlima litahusisha baadhi ya viongozi mashuhuri  wa jeshi Wastaafu akiwemo aliyekuwa mkuu wa majeshi ili kuhamasisha Watanzania waweze kupanda mlima ambapo tukio hilo litajulikana kama Uhuru Epedition .

Kijazi alifafanua kuwa pamoja na kuadhimisha uhuru wa nchi ,lakini madhumuni mengine ya zoezi hilo ni kuhamasisha utalii na kuhimiza uhifadhi wa mazingira kwani bado watanzania wengi hawana muamko wa kutembelea vivutio vya utalii hivyo kujikuta asilimia kubwa ya watalii ni kutoka nje ya nchi.

"Katika maadhimisho haya tuna malengo ya kuhamasisha watanzania ili wajitokeze kupanda mlima kilimanajaro pamoja na kutembela hifadhi mbali mbali, kwani tunavyo vivutio 16 ambavyo vipo ndani ya tanzania na vinahitaji watanzania wote wanufaike navyo sio tu wageni kutoka nje ya nchi bali hata wa hapa wajue wanazo fursa "aliongeza kijazi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa zara Zainabu Ansell alisema kuwa Watanzania wanapaswa kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo la kihistoria kwani  wengi wao wamekuwa na mawazo potofu ya kufikiria wanaopaswa kupanda mlima na kutembelea hifadhi ni wazungu tu na wageni kutoka nje ya nchi hali inayowafanya watanzania kupoteza haki yao.
Kauli mbiu ya zoezi la kupanda mlima kilimanjaro mwaka huu ni endelea kuweka mazingira safi na salama ya fahari ya afrika.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Zara Tours Zainabu Anselm akiongea juu ya kampuni yake ambapo aliwataka wananchi wajitokeze kwa wingi kutembelea vivutio vilivyopo ndani ya nchi yetu na sio kuendelea kuviona kwa mbali tu na kuvisikia.
Meneja Utalii na masoko wa Tanapa Ibrahimu Musa, katikati ni Mkurugenzi wa Tanapa Allen Kijazi wa kwanza kushoto ni Afisa uhusiano wa Tanapa Paschal Shelutete

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...