Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
SERIKALI imesema itaendelea kuwaunga mkono watu wenye viwanda ili nchi iweze kufikia malengo ya uchumi 2020. 
Hayo ameyasema Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charle’s Mwijage wakati wa ufunguzi wa maonesho ya viwanda yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. 
Mhe. Mwijage amesema kuwa watanzania umefika wakati wa kujenga viwanda kuanzia viwanda vidogo hadi vikubwa kutokana na serikali kuweka mazingira bora katika sekta ya viwanda. 
Waziri Mwijage amesema kuwa viwanda vidogo sio vya kubeza hata kidogo kwani  nchi mbalimbali duniani zilianza na viwanda vidogo na vikawa vinachangia sehemu kubwa ya pato la mataifa yao.
 Amesema serikali itavilinda viwanda vilivyopo na vinavyojengwa kutokana na viwanda hivyo vinaajiri watanzania pamoja na pato la taifa kukua kwa viwanda hivyo, na ametaka maonesho hayo yalete mafanikio kwa maonesho yajayo. 
Mhe. Mwijage amesema watu walionyesha nia kujenga viwanda ni wengi hivyo matarajio ya nchi ya viwanda yakawa yameafikiwa na  serikali ya awamu ya tano kwa vitendo
Maonesho ya Viwanda vya Tanzania yameandaliwa na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kupitia taasisi yake ya mamlaka ya maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) na kujumuisha  viwanda vidogo, vya kati na vikubwa kushiriki maonesho hayo kwa kwanza ya aina yake kuanzia  tarehe 7 hadi 11 Desemba, 2016 katika viwanja vya (SabaSaba) Mwalimu J.K Nyerere, Barabara ya Kilwa, Dar es salaam. Takriban viwanda 400 vinashikiri na kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bw. Edwin Rutageruka yatafanyika kila mwaka wakati kama huu ili kuunga mkono na kusisimua azma ya Serikali ya awamu ya Tano kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ili kuongeza kasi ya maendeleo.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji,  Mhe. Charle’s Mwijage akizungumza katika ufunguzi wa maonesho ya viwanda yanayofanyika katika viwanja vya sabasaba  barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

 Kaimu Mkurugenzi wa TanTrade,  Edwin Rutageruka  akizungumza juu maonesho ya viwanda leo katika viwanja vya Saba Saba  barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya hadhira  wakimskiliza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charle’s Mwijage wakati akifungua maonesho hayo katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charle’s Mwijage akiambatana na Kaimu Mkurugenzi wa TanTrade Bw.  Edwin Rutageruka kutembelea mabanda. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...